Utata wa ajira mpya za walimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata wa ajira mpya za walimu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by TEMILUGODA, Feb 18, 2012.

 1. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Watanzania wengi tumefurahi kwa shule zetu kupata walimu watakao punguza mass failure kwa watoto wa kitz,lakini je tunajua utata ndani ya ajira hizo,nakupeni kwa uchache tu; 1.walimu wa zamani waliokuwa masomoni wameajiriwa upya 2.walimu wa zamani wame wametoweka na kwenda kwenye vituo vipya[jiulize kwa nini] 3.walimu hawa wakongwe walipoajiriwa awali walilipwa subsistence allowance na sasa tena wamelipwa[double payments] 4.walimu wapya si 23,000 bali ni pungufu ya hapo[sijapata mantiki ya hakiki za watumishi zinazofanywagwa hapa tz kama zinaumakini au hufanywa kwa uzoefu tu.] Nawasilisha naomba tuchangie
   
 2. MAKOLE

  MAKOLE JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 601
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  hilo ni kwa sababu ya uzembe wa serikali...kwa mfano. huyo fresh from school akianza kulipwa mshahara wa shilingi 10 za kitanzania wakati yule in service aliondoka kituoni huku analipwa shilingi 5 na kuongezeka hadi sh. 6 za kitanzania ataanzia mshahara wake hapo....sasa ni hivi rhusa yenyewe kapata kwa tabu 2, ofisi haijampa hata sarafu nyeupe ya Tsh1. la 3. kasoma kwa tabu kubwa sana, si ajabu hata mshahara alishatemwa, 4. mkopo alitoswa 5. hata akirudi ofisi hawatambui elimu yake hadi alete cheti halisi cha shule, sio result slip ama transcript kwa shahada...6. hata akileta hicho cheti leo, itamchukua hadi 2 years kubadilishiwa cheo kipya, na sio kulipwa mshahara mpya....Kwa hali hiyo.. hata ingekuwa ni mimi ningesepa ili nikaanze na mshahara wa juuu baba......tunahitaji kuishi leo na sio kuishi kesho mkuu..
   
 3. M

  MZAWATA JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Makole umenena na nakuunga mkono kwa 100%
   
 4. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Mod naombwa thread hii iwekwe hapa ili ipate kuchangiwa.
   
 5. Chilli

  Chilli JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 17, 2011
  Messages: 1,638
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Umemaliza kazi mkuu. Sababu kuu ya walimu kwenda vituo vipya nz kukimbia vya zamani ni ubabaishaji uliopo kwenye hii wizara pamoja na roho mbaya za maafisa elimu (W) na baadhi ya wakuu wa shule. Kila mtu anatafuta green pasture bana.
   
 6. Mwita Matteo

  Mwita Matteo JF-Expert Member

  #6
  Feb 19, 2012
  Joined: May 16, 2010
  Messages: 216
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ndugu unachojaribu kukiongelea hapa mimi kidogo kimenitatizo na jua kuna tatizo lilitokea Wizara ya Elimu kufanya re-alocation nkimaanisha kuna baadhi ya walimu waliomaliza chuo mwaka 2010 na kupangiwa vituo mwaka 2011 walipangiwa vituo tena mwaka huu 2011, ila walimu hao ni waliosoma Chuo Kikuu Kishiriki Cha Elimu Mkwawa, na baada ya kuligundua hilo wiizara ilyaondoa majina hayo, na kurekebisha, sasa hao walliopangiwa na kuacha vituo vyao na kwenda kwenye vituo vipya sina uhakika kama wanaweeza kupata double payment, kwa kuwa majina yao yapo katika database ya hazina na vilevile kama ni mkongwe kama ulivyosema atakuwa anajipotezea muda kwasababu ataanzia mshahara amabao tiyari atakua kesha upita
   
 7. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  mleta mada fanya uchunguzi, walimu crash/voda fasta waliokua wameajiriwa kwa leseni wote hawakupangiwa vituo baada kumaliza chuo mwaka jana. Waliopata vituo mwaka huu ni wale pre service na sio inservice.
   
 8. M

  Mwanyava JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 206
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hata inservice wamepata ajira mpya. Sijajua unachobisha hapa ni kipi. Mfano mmoja nitakupa nao ni huu: mdogo wangu alikuwa mwalimu shule ya msingi, kajiendeleza mpaka kidato cha sita na baada ya hapo kaenda chuo na kamaliza stashada mwaka jana na kurejea kituo chake cha kazi. Lakini jina lake limo kwenye ajira mpya na kapangiwa mkoa wa Mbeya. Huyu ni mmoja tu watakuwepo wengi wa namna hii na pia wale walio jiendeleza kutoka stashahada kwenda shahada ya kwanza nadhani nao watakuwa wamepata ajira mpya.
   
 9. T

  TEMILUGODA JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Wewe ndo huna data data,ungetaka kujua ingia kwenye mtandao halafu tafuta ajira za walimu walimu mwaka 2005-2007 matharani,kisha nakiri majina hayo vizuri halafu tena fanya hivyo kwa ajira za mwaka huu utagundua.PILI tunawaona walimu waliopata haya mambo[siwezi kutaja majina kwa sababu].Cha msingi jambo hili lipo na ni la kweli kama wachangiaji wengine walivyo justify!
   
 10. M

  Mayongeyonge Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mimi niliajiriwa tena shinyanga ila sijaenda.hili linatokana na wizara kubase na data za chuo tu bila kucheki na data za utumishi
   
Loading...