Utata: Mwenyekiti wa CCM taifa anateuliwa au kuchaguliwa na wajumbe?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
40,334
72,798
Kuna kauli nyingi kuwa mkutano maalum wa CCM utaitishwa "kumkabidhi" chama Rais Magufuli ili awe mwenyekiti baada ya JK kuamua kujiuzulu kumpisha kama desturi ya chama hicho.

Katiba ya CCM inaonyesha mwenyekiti wa chama anachaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama, lakini kwa maelezo na mwelekeo inaonyesha kuwa kinachotaka kufanyika ni 'kumkabidhi' uongozi Rais Magufuli na sio kufanya uchaguzi kumchagua kuwa mwenyekiti.

Kwa hali ilivyo sasa hivi ya "Tumpe, Tusimpe" itakuwaje kama katika hao wajumbe zaidi ya 3000 wakipiga kura na 2000 wakisema HAPANA?

Jee itabidi itumike njia ileile inayofahamika ya kugeuza matokeo na kuminya uhuru wa wana ccm kuchagua kiongozi wao au kumkataa mtu?

Nini hatima ya chama baada ya hiyo 2/3 uamuzi wao kuchinjiwa baharini?
 
Watangaze kila mwana Ccm anayeutaka uenyekiti wa taifa aombe....pia wajieleze mbele ya wanachama bila kukatwa.....lazima atatokea mmoja wa kumchana laivu mtarajiwa
 
Mkuu asihangaike Na hilo tutatumia njia kama iliyotumika kumpitisha Lowasa kugombea Urais kupitia Chadema pale karmjee.

Shida iko pale ambapo kuna sintofahamu ya "Tumpe au Tusimpe". Jee kama ikitokea wanaosema Tusimpe kuwa wengi inakuwaje?
 
Kuna kauli nyingi kuwa mkutano maalum wa CCM utaitishwa "kumkabidhi" Chama Rais Magufuli ili awe Mwenyekiti baada ya JK kuamua kujiuzulu kumpisha kama desturi ya chama hicho.
Katiba ya CCM inaonyesha Mwenyekiti wa Chama anachaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu wa chama, lakini kwa maelezo na mwelekeo inaonyesha kuwa kinachotaka kufanyika ni 'kumkabidhi' uongozi Rais Magufuli na sio kufanya uchaguzi kumchagua kuwa mwenyekiti.
Kwa hali ilivyo sasa hivi ya "Tumpe, Tusimpe" itakuwaje kama katika hao wajumbe zaidi ya 3000 wakipiga kura na 2000 wakisema HAPANA? Jee itabidi itumike njia ileile inayofahamika ya kugeuza matokeo na kuminya uhuru wa wana ccm kuchagua kiongozi wao au kumkataa mtu?
Nini hatima ya chama baada ya hiyo 2/3 uamuzi wao kuchinjiwa baharini?
Ya mgombea wa ukiwa umesahau au hukuliona?
 
Shida iko pale ambapo kuna sintofahamu ya "Tumpe au Tusimpe". Jee kama ikitokea wanaosema Tusimpe kuwa wengi inakuwaje?
2015 wengi walisema "tumpe"...wachache wakasema "akatwe"...na mpaka sasa, chama kipo imara than ever before...
 
Back
Top Bottom