Utata mauaji ya Mwangosi na hukumu yake

Utata mauaji ya Mwangosi na hukumu yake

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,737
Reaction score
14,894
"Sikuweza kutambua chochote kama kuna kitu kilitokea lakini Septemba 3/2012 niliona gazeti ofisini kwa RPC(kamanda wa polisi wa mkoa) Kamuhanda, ndipo nilibaini kuna kitu kilitokea jana yake.
Baada ya hapo tulizifatilia kwa mtu mmoja mmoja kuanzia kwa wale askari walionekana kwenye picha hadi kumbaini mtuhumiwa".
Maelezo ya shahidi wa kwanza, Said Mnuka ambaye ni afisa wa FFU aliyoyatoa mbele ya jaji Paulo Kihwelo 12/2/2015
MWANGOSI.JPG

‪‎Mwanzo_wa_utata_huu_hapa‬.
"Siku hiyo nilitekeleza maagizo niliyopewa na Kamanda Kamuhanda(RPC Iringa) ambaye aliniagiza nielekee nikiwa na kikosi changu.
Tulitoka na gari moja la mkoa, magari mawili ya FFU kutoka dodoma.
Tulipofika Mufindi tulikutana na magari mawili ya FFU kutoka Mufindi tukaungana na kuelekea eneo la tukio.
Tulipofika tuliwakuta Chadema wamefunga vipaza sauti tayari kwa kuanza mkutano.
Nilitelemka kwenye gari na kuongea na viongozi wa Chadema lakini walikataa na kutamka liwalo na liwe, lazima wafanye mkutano.
Tuliwatawanya kwa mabomu na baada ya fujo kutulia ndipo tuliamriwa kuingia kwenye magari kurudi kambini.
Wakati nikiingia kwenye gari ndipo alipotokea Mwangosi na kunikamata mikono bila ya kujua dhumuni lake ndipo nilipopiga kelele kuomba msaada kwa askari wenzangu.
Wakati askari wakiendelea kunisaidia, nilisikia mlipuko wa kishindo kikubwa na kupoteza fahamu.
Nilipozinduka nilijikuta nimelazwa hospitali ya wilaya ya Mufindi bila ya kujua kilichotokea Septemba 2".
Maelezo ya shahidi namba mbili, Assel Mwampamba ambaye alikuwa mkuu wa polisi wa wilaya(OCD) Mufindi.
‪Mtuhumiwa_ajutia_kumuua_Mwangosi‬.
"Mtuhumiwa(PC Pacific Cleofas Simon) aliletwa kwangu kuungama kwa kumuua Mwangosi kwa bomu bila kukusudia.
Aliletwa kwangu kuungama wakati nikiwa hakimu Mahakama ya Mwanzo Iringa Septemba 5,2012 saa 7:24 mchana.
Nilimkagua mtuhumiwa mwilini na kumkuta na jeraha bichi mkono wa kulia katika kidole cha kati.
Nilipomuuliza kuhusu jeraha hilo, aliniambia aliumia wakati bomu lilipolipuka".
Maelezo ya shahidi namba tatu, Frola Mhele ambaye ni hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Dodoma aliyoyatoa Februari 16/2015.
IMG_1919.JPG

‪Bunduki_iliyomuua_Mwangosi_hii_hapa‬.
"Siku ya tukio nilipokea simu kutoka kwa mkuu wa FFU, Said Mnuka saa 12:30asubuhi akiniita haraka katika ghala la Siraha akinieleza kuna dharura imetokea Mufindi hivyo anahitaji siraha.
Bunduki ya mtuhumiwa(Pacificus Simon) ilikuwa na namba 040824.
Alitoka na mabomu 15 ya kishindo kikubwa, mabomu 22 ya moshi ya kurusha kwa mkono na risasi 60 za bunduki ya SMG ambazo hazikurudi hata moja".
Maelezo ya shahidi namba nne, Lewis Tiekya ambaye ni mtunza ghala la siraha msaidizi.
‪‎PC_Pacific_Simon_katolewa_kafala‬?
Ukifatilia mlolongo mzima wa usikilizwaji wa kesi ya mauaji ya Mwangosi hadi hukumu iliyotolewa hapo jana(Julai 27,2016) na Mahakama Kuu Kanda ya Iringa ya kumtia hatiani PC Pacificus Simon na kumuhukumu kifungo cha miaka 15 kwa kosa la kumuua Mwangosi bila kukusudia lazima utagundua utata katika kutambuliwa kwa mtuhumiwa.
Ukiangaliwa picha iliyopigwa eneo la tukio utabaini kulikuwa na askari zaidi ya wanne ambao wanaonekana wakimpiga Mwangosi kabla ya kifo chake, swali la kujiuliza ni kwanini wale askari wengine hawakukamatwa?
4.jpg

Kwanini RPC Kamuhanda hakuwajibishwa katika hili licha ya kuwepo eneo la tukio na kushudia Mwangosi akiuwa na badala yake alipandishwa cheo? RPC Kamuhanda alifatwa na baadhi ya waandishi wa habari wakimuomba awaamuru askari wake wamwache Mwangosi lakini alipandisha kioo cha gari, je alikuwa anakubaliana na walichokuwa wanakifanya askari wake?
Kama OCD Assel Mwampamba alifahamu Mwangosi ni mwandishi wa habari, kwanini hakuwazuia askari wake wasimuue Mwangosi wakati yeye(OCD Assel) alikuwa 'Operation Commander Incharge'?
Pc Pacificus Simon anajitetea kuwa bomu lililipuka kwa bahati mbaya kutoka kwenye bunduki yake, inawezekanaje bomu lilipuke kwa bahati mbaya wakati anajua utalatibu wa bunduki ni kuweka 'usalama OFF' inapokuwa haitumiki au 'ON' inapokuwa inatumika?
Je PC Simon alifanya hivyo? Kama aliweka ON kwanini hakuelekeza mtutu wa bunduki chini kama tahadhari?
2a.JPG

Kwanini mara zote mtuhumiwa alipokuwa anafikishwa mahakamani waandishi wa habari walizuiwa wasimpige picha kama utalatibu unavyoruhusu?
Nani aliwaagiza wale polisi watatu wamficha mtuhumiwa na kumfunika shuka la kimasai wakati anaingia mahakamani kusikiliza hukumu yake hapo jana?
Nani anaifahamu sura ya mtuhumiwa?
Kufichwa huku kwa sura ya mtuhumiwa si 'privallege' aliyofanyiwa na polisi wenzie baada ya kukubali kuwa mbuzi wa kafara katika kesi ya mauaji ya Mwangosi?
MWENYEZI MUNGU AMUHIFADHI MAHARA PEMA PEPONI MWANGOSI
 
Risasi 60 za SMG hazikurudi hata moja? Huyo ni Askari mmoja. Je kwenye matukio kama haya hakuna uwezekano wa Askari kujihusisha na Biashara haramu ya Risasi kwa kigezo kwamba zilitumika kwenye tukio?
 
Huo mwili wa marehemu jamani dah, masikini apumzike kwa amani.....
Yaani walimfumua kifua na utumbo laivu kabisa. Sijui bomu gani hili walitumia. Mungu yupo lakini hata ng'ombe hastahili kuuliwa namna hii. Huyo Kamuhanda sidhani kama ana amani huko aliko. Hata atakapostaafu na kuzeeka dhambi hii haitamwacha yeye na vizazi vyake vyote. RIP Mwangosi.
 
Yaani walimfumua kifua na utumbo laivu kabisa. Sijui bomu gani hili walitumia. Mungu yupo lakini hata ng'ombe hastahili kuuliwa namna hii. Huyo Kamuhanda sidhani kama ana amani huko aliko. Hata atakapostaafu na kuzeeka dhambi hii haitamwacha yeye na vizazi vyake vyote. RIP Mwangosi.
alaaniwe kabisa huyu kamahunda.....
 
Senga, Senga, Senga, Senga, umekwenda, Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua, Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga, Senga, kamsalimie Daudi Mwangosi, mwabie aliyemuua naye kahukumiwa jela miaka 15, kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu. Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.
 
Tukichunguza kifo cha Mwangosi kwa umakini tunaona chanzo chake kikiwa ni mawazo ya kipuuzi tu ya kutumia nguvu isiyostahili kupambana na mikusanyiko isiyo halali. Akili ya kawaida inaonesha majuto kwa jeshi la polisi na hata viongozi wengine wenye akili nzuri. Hata hivyo itakuwa vigumu kukiri makosa hali itakayosababisha wanaokusanyika bila uhalali (kulingana na tafsiri ya polisi) kuzidisha vitendo vyao. Hata hivyo, ni muhimu kifo hiki kiwe fundisho kwa wote waliohusika. RIP Mwangosi.
 
Yaani walimfumua kifua na utumbo laivu kabisa. Sijui bomu gani hili walitumia. Mungu yupo lakini hata ng'ombe hastahili kuuliwa namna hii. Huyo Kamuhanda sidhani kama ana amani huko aliko. Hata atakapostaafu na kuzeeka dhambi hii haitamwacha yeye na vizazi vyake vyote. RIP Mwangosi.
Mtunza ghala amesema yalikuwa mabomu "ya kishindo kikubwa"
 
Nimeangalia sana mwili wa huyu kaka. nachoweza kusema tu ni kwamba aliyeamuru na anayeunga mkono na anayekwepesha ukweli mpaka sasa ajue vita ni vya Mungu.Na kisasi ni cha Bwana.Yupo na anaweza.
Hii damu haitapotea bure.
Tuache mara moja matumizi ya nguvu yasiyo ya lazima.

RIP brother.Polen familia ambayo mnakosa huduma na mapenzi yake.Poleni jamii kwa kukosa mchango wake pia
 
Senga, Senga, Senga, Senga, umekwenda, Mungu aliamua akuweke hai mpaka hukumu itoke na mwisho amekuchukua, Senga umekwenda wadogo zako katika tasnia tukiwa na hamu ya kujifunza kutoka kwako.
Senga, Senga, kamsalimie Daudi Mwangosi, mwabie aliyemuua naye kahukumiwa jela miaka 15, kamwambie mazingira ya waandishi wa habari bado magumu. Nenda Senga, picha zako zinabaki kuwa rejea ya mafunzo ya uandishi wa habari katika mazingira hatarishi.
...wewe ni Dotto?
 
Kama walimficha uso...je utajuaje kama hajafungwa kweli? Nani atazibitisha kwamba aliefungwa ndiyo uyo wakati hakuna aliemuona?
 
Back
Top Bottom