CHA The GREAT
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 651
- 854
Kuna taarifa zimeenea kuanzia jana kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John P. Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani na taasisi ya Nelson Mandela. Mbali na Rais Magufli wengine waliotunukiwa tuzo toka taasisi hiyo ni pamoja na Pierre Nkurunzinza ambaye ni Rais wa Burundi na Uhuru Kenyatta.
Kuna mashaka na taarifa hiyo kwa sababu zifuatazo kama zilivyoainishwa:
Kwanza, chanzo cha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa facebook, ni chanzo ambacho hakijahakikiwa (verified) kama ilivyo vyanzo vingi vya kuaminika.
Pili, hakuna chombo kingine cha habari kilichoripoti habari hiyo licha ya umuhimu wake.
Tatu, website: www.institutmandela.com ambayo ndiyo inayoonesha kuhusiana kwa ukaribu na tuzo za taasisi ya Mandela, haina taarifa kama hiyo kuhusiana na utolewaji wa tuzo hizo.
Nne, kwa mara ya mwisho, tuzo hizo zilitolewa mwezi November, 2017. Inakuwa vigumu kuamini kwamba taasisi moja inaweza kutoa tuzo mara mbili kwa mwaka huo huo (mtanisahihisha kama nakosea).
Kama kuna mtu ana chanzo cha kuaminika na atuletee hapa ili kuondoa sintofahamu hii kwa ajili ya kutoa taarifa zilizo sahihi na zisizo na mashaka.
Tukio la wanahabari wa TBC miezi kadhaa iliyopita kutangaza habari ya uzushi kwamba, Rais Donald Trump amesifu jitihada za Rais Magufuli, zinafanya sintofahamu hii kuibuka kutokana na kutokuonekana kwenye vyombo vya habari vingine.