Utashi wa kisiasa na maendelea ya kisayansi katika nyanja za tafiti

procura

Member
Jul 14, 2013
34
25
Tafiti ndo njia pekee ambayo mataifa yaliyoendelea huamin katika kutambua matatizo na suluhusho ya hayo matatizo. Ni kwa msingi huo, haya mataifa yamekuwa yakiwekeza zaidi katika tafiti kwa kutumia vyuo vyao vikuu. Makampuni mengi ya kimataifa nayo yamekuwa yakifadhili tafiti hizo kwa sababu matokeo ya tafiti huyanufaisha zaidi hayo makampuni. Kwa mfano katika nchi ya uingereza zaidi ya asilimia 40 ya udhamin wa tafiti hutoka kwenye makampuni yasiyo ya kiserikali.

Katika nchi yetu ya Tanzania serikali haiipi kipaumbele sana udhamin wa tafiti, katika tafiti zote zinazofanyika nchini, ni asilimia moja tu ndio hudhaminiwa na serikali lakin nyingi hutoka kwenye makampuni ya nje au mashirika ya misaada toka nchi za ulaya na marekani. Chanagamoto ya tafiti zinazodhaminiwa na mashirika toka nje ni kuwa mara zote wao ndo huamua aina gani ya tafiti wanazihitaji tegemea na matumizi ya matokeo ya tafiti hizo katika nchi zao na makampuni yao. Hali hii ndo inasababisha kuonekana tafiti nying zinazofanyika nchini hazina manufaa kwa wanachi, lakini kiukweli zina manufaa sana kwa wazungu ambao ndio wanaozifadhili kwa kutegemea na uhitaji wao, na mara zote watafiti wanatakiwa kuto mwenendo wa tafiti tangia mwanzo wa tafiti hivyo wazungu wanapata matokeo yote na wanayatumia kwa manufaa ya makampuni yao.

Je ni kweli nchi kama nchi inaamin katika tafiti hususani za kisayansi? Je kuna utashi wa dhati angalau kutenga asilimia tano tu ya bajeti ya nchi kwa ajili ya tafiti kwa kutumia vyuo vikuu vya serikali kama Muhimbili, SUA na UDSM? Je serikali inajua kuwa tafiti hizi zinaweza kuzalisha wataalam waliobobea wengi kwa sabab hizi zitaenda sambamba na kusomesha wanavunzi katika ngazi za masters na PhD? Hivi serikali inajua wanataaluma wanahangaika kuandika proposals kutokana na objective za wazungu ili tu wapate funds kwa sabab tu serikali imejitoa katika udhamin wa tafiti?

Kama kweli tunahitaji maendelea basi lazima tuwekeze kwenye sehem sahihi ili kuepusha ana ana doo katika kutimiza ajenda zetu kama nchi. Yapo mashirika mabayo udhamin wao labdo ni bilion tatu lakin unazalisha wataalam katika ngazi za phD na masters zaidi ya 100. Serikali iamua kutatua matatizo yake kwa kutumia tafiti za wataalam wa ndani sio kupokea tafiti toka kwa wazungu na kupangiwa dawa za kutibu, mbegu za kupanda. WAKATI NI SASA
 
Back
Top Bottom