Amicus Curiae
JF-Expert Member
- Sep 12, 2012
- 4,809
- 6,342
Habarini za wakati huu wakuu..
Moja kwa moja kwenye mada. Inawezekana nia ya Serikali ni njema, lakini tatizo liko kwa watendaji waliokabidhiwa ofisi za Serikali kuwahudumia wananchi.
Kuna mti wa mwembe umeegamia kabisa uzio wa jirani yetu in such a way kwamba wazoefu wanasema muda wowote kuanzia sasa unaweza kuangukia upande wa huyo jirani yetu na kusababisha maafa.
Tulipotaka kuukata tukadokezwa kwamba siku hizi huruhusiwi kukata wala kupunguza matawi mti wowote bila kibali, vinginevyo kuna fine, achilia mbali MVULE ambao inafahamika tangu zamani kwamba hautakiwi kukatwa bila kibali maalumu.
Kweli nimefika hadi ofisini kwa Mtendaji wa Mtaa, akaniambia nimuandikie barua ya ombi la kukata huo mwembe. Nikaiandika. Shida ikaanzia hapa, akasema anatakiwa aitishe kikao cha wajumbe wa Serikali ya Mtaa kujadili agenda ya kukata huo mwembe! Yani mti unapangiwa agenda na wajumbe wa Serikali ya Mtaa! Wajumbe wako 7 kwahiyo niwatafutie posho kwasababu wakiitwa wataacha shughuli zao kuja kikaoni. Hivi, hizi nafasi za ujumbe wa Serikali za Mtaa si mtu anaomba kwa hiari? Kwanini aombe kama ana shughuli nyingine?
Shida siyo kutoa posho, shida ni Mtendaji anavyolazimisha!! As if bila posho mti haukatwi hata kama hali yake ni hatarishi kiasi gani!!!
Haya..wakishakaa wajumbe barua inaenda kwa Afisa Mazingira wa Wilaya, anaiidhinisha. Hatua inayofata barua inaenda kwa DAS, naye atoe kibali, na hatua nyingine ambazo sikuwa interested kuzisikiliza.
Wakuu, niko kwenye nafasi ya kutoa malalamiko yangu ngazi za juu na huyu Mtendaji akawajibishwa lakini sioni haja ya kufanya hivyo, naamini humu ndani kuna maafisi wa kada mbalimbali wa Halmashauri za Miji na Majiji, hebu tusaidiane katika hili.
Sawa kuna njaa mtaani, lakini hii haiwezi kuwa sawa. Kwahiyo wale masikini hawataruhusiwa kukata miti waliyoipanda na kuihudumia wao wenyewe kwa kukosa posho ya kikao cha wajumbe?
Tutamkumbuka sana JPM. Naombeni ushauri tafadhali...