Utaratibu wa kuitwa kituo cha polisi

Utaratibu wa kuitwa kituo cha polisi

nusuhela

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
6,270
Reaction score
7,768
Samahani, ningependa kujua utaratibu wa mtu kuitwa kituo cha polisi

Ipo hivi, leo mida si mirefu, nimepokuta missed call kwenye simu yangu. Nilipopiga, nikauliza mwenzangu nani maana nimekuta missed call?
Ndipo alipojitambulisha kuwa ni askari kutoka kituo fulani cha polisi. Hivyo inatakiwa nifike jioni maana kuna jambo limetokea.

Shida yangu ipo kwenye utaratibu wa kuitwa kituo cha polisi maana sijawahi kuitwa. Je, inatakiwa nikipigiwa simu na mtu nisiyemjua akaniambia niende kituoni inabidi niende au unaweza ukawa mchezo? Maana najaribu kujiuliza ni wapi nimekosea mpaka niitwe kituoni sioni.

Naomba msaada wa maelekezo yenu
 
Polisi hutumia pia mbinu hiyo kuita mtu kituoni, hivyo ni vema ukauliza kuna tatizo gani huko ili uende ukifahamu? Kuna jamaa ilitokea kama wewe kukuta Missed Call.

Alipopiga aliambiwa anaitwa Polisi, akauliza kuna shida gani? Askari akamjibu kuna shtaka la shambulio kwa mkewe. Ndipo akaaenda polisi.
 
Acha uoga..wewe kama umayavagaa nenda kasolve
Kwamba umeshindwa kuuliza kwanini wanakuita???
 
Uende na mtu wa dhamana kabisa la sivo utalala ndani kimasikharaa ilinitokea juzii
 
Samahani, ningependa kujua utaratibu wa mtu kuitwa kituo cha polisi

Ipo hivi, leo mida si mirefu, nimepokuta missed call kwenye simu yangu. Nilipopiga, nikauliza mwenzangu nani maana nimekuta missed call?
Ndipo alipojitambulisha kuwa ni askari kutoka kituo fulani cha polisi. Hivyo inatakiwa nifike jioni maana kuna jambo limetokea.

Shida yangu ipo kwenye utaratibu wa kuitwa kituo cha polisi maana sijawahi kuitwa. Je, inatakiwa nikipigiwa simu na mtu nisiyemjua akaniambia niende kituoni inabidi niende au unaweza ukawa mchezo? Maana najaribu kujiuliza ni wapi nimekosea mpaka niitwe kituoni sioni.

Naomba msaada wa maelekezo yenu
Kimbia mbio tena wahi maana kwanza wamekuheshm sna had kukupigia vinginevo wangekudaka juu kwa juu na aibu kibao
 
Back
Top Bottom