Utaratibu wa hospitali ya Sekou Toure kuhoji maradhi hadharani haufai

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kisheria maradhi ya mgonjwa ni siri ya mgonjwa mwenyewe na hatimaye daktari anayemtibu ambaye naye hana haki ya kumueleza mtu mwingine yeyote bila idhini ya mgonjwa husika.

Lakini nimekuwa nikisikitishwa na utaratibu wa hospitali ya Sekou Toure usiokuwa wa siri wala faragha ya maradhi ya mgonjwa.

Leo hii nikiwa katika foleni ya kupata kadi ya matibabu nimeshuhudia ikimwia ngumu mama mmoja wa makamo kueleza ugonjwa wake baada ya kutakiwa aeleze tena mbele za wagonjwa wengine wa jinsia tofauti tofauti.

Utaratibu huu ambao kusudi lake huwa ni kujua aina ya maradhi ili mgonjwa aelekezwe daktari husika wa tatizo la mgonjwa, kwa kweli si rafiki sana wa wagonjwa, kwa hiyio tungeomba sana utaratibu huu ubadilishwe kwa sababu katika hali ya mkusanyiko wa aina ile si vema mgonjwa kuanika maradhi yake.
 
Back
Top Bottom