Utaratibu NSSF

Utaratibu NSSF

Joined
Mar 25, 2022
Posts
28
Reaction score
34
Wakuu naombeni maelekezo juu ya hili, mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni binafsi baadae nikaacha kwa hiari yangu, kwenye account yangu ya NSSF kuna kiasi changu kadhaa cha pesa, sasa nahitaji nijue nifuate utaratibu gani ili kuipata, na naweza kuipata ndani ya muda gani kama nikianza mchakato??
 
Kwa vile umeacha kazi mwenyewe hupati kitu ndugu.
 
Kwa hiyo ili upate hiyo hela ni vigezo gani unatakiwa, kuwa sehemu nimewahi kumbiwa nikiwa na barua kutoka kwa muajiri inaweza kusaidia, hili lipoje?
 
Wakuu naombeni maelekezo juu ya hili, mimi nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni binafsi baadae nikaacha kwa hiari yangu, kwenye account yangu ya NSSF kuna kiasi changu kadhaa cha pesa, sasa nahitaji nijue nifuate utaratibu gani ili kuipata, na naweza kuipata ndani ya muda gani kama nikianza mchakato??
Zamani tulikuwa tunawasilisha barua ya kutoka kwa mwajiri wako ulikotoka ya kuacha au kuachishwa kazi,
ukiacha kuna barua unamwandikia mwajiri na yeye anakujibu. Au ukifukuzwa kuna barua unapewa na mwajiri.
Walikuwa wanashauri usubiri miezi 6 ili kuona kama utapata ajira nyingine.

Hiyo barua ndo unaipeleka NSSF nao wanakupa fomu ambazo unampelekea mwajiri wako,
ambaye anakujazia kuonyesha alivyokuchangia kwa kuonyesha namba za lisiti za mlipo aliyopelekea michango
yako. Hiyo fomu ikishajazwa unairudisha NSSF wanakwambia muda wa kusubiri ili malipo yako yawe yameandaliwa.
Huo muda ukifika unaenda unapewa cheki yako.

Baada ya zile figisu za yule mkurugenzi aliyetumbuliwa na mh.JPM na sheria kandamizi
zilizotungwa baada ya hapo,sijui taratibu kama zimebadilika au bado ni zile zile.
Mimi kwa utaratibu wa hapo juu nilifanikiwa kuchukua mafao yangu mara mbili,
kabla ya kufikisha umri wa miaka 45.na nikiri kwamba utaratibu ule ulikuwa unasaidia sana
kwa wapambanaji tunaobebwa na juhudi zetu binafsi.
 
Ukipeleka barua ya ku resign hautapata kitu, kama unaweza kuongea na mwajiri wako akupe barua ya kukuachisha kazi itakusaidia. Kama huwezi kupata barua ya kuachishwa kazi ifoji ili maisha yaendelee.
 
Ukipeleka barua ya ku resign hautapata kitu, kama unaweza kuongea na mwajiri wako akupe barua ya kukuachisha kazi itakusaidia. Kama huwezi kupata barua ya kuachishwa kazi ifoji ili maisha yaendelee.
Duh, ila inaonyesha mizunguko ipo ya kutosha
 
Nenda Nssf kachukue fomu .. (hakikisha uwe umekaa miezi 6 baada ya kuacha kazi)
Fomu itakuelekeza ni vitu gani uambatanishe.. mara nyingi huwa

1.passport tatu
2.bank statement
3.certificate baada ya kuacha/kuachishwa kazi
4.coppy ya kitambulisho cha mpiga kura au nida
5.copy ya kadi ya uanachama
6.barua ya kuacha/kuachishwa kazi..
7.copy ya mkataba wako wa kuanza kazi
 
Ni mwezi mmoja tu sio 6
 
Kwa hiyo ili upate hiyo hela ni vigezo gani unatakiwa, kuwa sehemu nimewahi kumbiwa nikiwa na barua kutoka kwa muajiri inaweza kusaidia, hili lipoje?
Kama una barua ya mwajiri inayoonesha lini ajira ilikoma au ukiwa na certificate of service ,nenda ofisi za nssf utapewa mwongozo.Achana na hearsay.AMRi
 
Kwa sasa utaratibu umebadilika kupata io ela ni mziki sana labda kama unataka asilimia 33.3 % ya mshahara wako wa mwisho kwa muda wa miezi 6. kama umechangia kwa muda wa miezi 18 na utapata asilimia 50% ya michango yako yote kama umechangia chini ya miezi 18 kwa mara moja io asilimia 50% ,kiukweli ni kanuni flani ambazo ni kandamizi sana kwa watafutaji ambao hawana taaluma
 
Pesa yakwako mwenyew umeipatia tabu bado kuipata tena upate tabu dah so fare kabisaa
 
Back
Top Bottom