Utaratibu mpya wa Sumatra wasotesha abiria bandarini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaratibu mpya wa Sumatra wasotesha abiria bandarini

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by abdulahsaf, Aug 15, 2012.

 1. a

  abdulahsaf JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 31, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h]  Mamia ya abiria waliotarajiwa kusafiri jana kwenda visiwani Zanzibar, jana walikwama kuondoka kutokana na utaratibu mpya wa vitambulisho unaodaiwa kutolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini Nchini (Sumatra).

  Kwa mujibu wa utaratibu, abiria haruhusiwi kukata tiketi ya kusafiri kwenda visiwani humo iwapo hatakuwa na kitambulisho, kikiwamo cha uraia.

  Vitambulisho vingine ambavyo abiria anatakiwa kuwa na kimojawapo, ni pamoja na cha makazi, kupiga kura, kazi, leseni ya dereva, utambulisho kutoka serikalini au pasi ya kusafiria.

  Baadhi ya abiria waliokwama kusafiri, walisema wamechelewa kupata taarifa hizo kwa kuwa hawaujasikia utaratibu huo katika chombo chochote cha habari.

  Utaratibu huo ambao maelezo yake yamebandikwa kwenye kuta za ofisi za kukatia tiketi katika bandari za meli zinazokwenda visiwani humo, umeelezwa kuwa ulianza kutumika rasmi Agosti 13, mwaka huu.
   
 2. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Tatizo vyombo au taasisi husika huendesha hutekeleza maamuzi yao kwa nguvu ya soda, kuna wakati kule Zanzibar ilikuwa huwezi kupata tiketi bila kitambulisho, lakini ilifanyika hivyo nafikiri labda ndani ya mwezi mmoja tu. SUMATRA wanapaswa kutoa elimu ya kutosha kwanini? mtu anhitaji kutoa utambulisho anapokata tiketi; vile vile inapotokea ajali wanapaswa kuchukua hatua kuhakiki wahanga wanafidiwa, hii itachangia kuonyesha umuhimu wa jambo hilo kwa jamii.
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,953
  Likes Received: 1,509
  Trophy Points: 280
  Na kama sina hivyo vitambulisho walivyosema hapo juu,kwani Tanzania hatuna vitambulisho vya raia ,hizo pasi kupata ni longolongo na lazima uwe na sababu ya maana,na vya udereva mimi hata baisikeli sina ,na hiyo mifuko ya jamii ndio usisesema mimi ni mchoma mkaa,sasa itakuwaje?je kwenda Mafia nako watadai hizo hati ,na je kwenda bukoba kupitia ziwa victoria au Ukerewe nako Sumatra wanadai hizo hati?basi hata Kigamboni iwe ni hivyo au ndio Zanzibar sio Tanzania?
   
 4. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Watanzania tuna matatizo na ni wataalam wa kulalamika kwelikweli.
  Hivi mnaosafiri kwa ndege airport mnafika saa ngapi? na kwa nini?
  Lack of identification ndiyo tatizo kubwa hasa wakati wa maafa kuwatambua waathirika
  SUMATRA baada ya kupewa majukumu na SMZ pamoja na SMT wameanzisha utaratibu unaoeleweka
  mmeanza kulalamika ooh nguvu ya soda ooh wanasumbua abiria come on guys mnataka nini hasa?
  Tunaweza kuleteana unazi wa kisiasa lakini kwenye element ya safety waacheni wataalam washughulikie mbona zamani zanzibar tulikuwa tunakwenda na passport?????
  What sort of society are we in YOU ARE DAMNED IF YOU DO AND YOU ARE DAMNED IF YOU DONT?
   
 5. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #5
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,064
  Trophy Points: 280
  Maoni yangu ni kuwa sisi kama wananchi nasi tunamatatizo ambayo kuna wakati tunalazimisha uvunjwaji wa sheria kwa sababu ya convenience tu. Mfano kwenye vyombo vya usafiri hata gari ikiwa imejaa tuko tayari kupanda eti kwa sababu ya uharaka wa safari zetu. wenye vyombo wanatambua hivyo na ndiyo maana tunateketea kila siku. dereva anaendesha vibaya lakini tukikutana na polisi njiani hatulalamiki na hata tukiulizwa kama dereva anaendeshaje katika safari response yetu ni passive.
  Vyombo kama Sumatra vinaudhaifu wake lakini na sisi wananchi hatusaidii kazi yetu ni kucriticise tu bila kutuo alternative option
   
 6. sister

  sister JF-Expert Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  utaratibu siyo mbaya ingawa nadhani walibidi watangaze ili watu wajue mana hata mimi binafsi huu usumbufu ungenikuta.

  ila nadhani sumatra waje hadi uku kwenye usafiri wa nchi kavu ( kwenye magari ya mikoani )mana tunalanguliwa sana ticket na watu wengi wana kasumba ya kuandika majina ya uongo kwenye ticket sijui kwanini na mwisho wa siku likitokea la kutokea inakuwa shida kuwatambua mana majina ya uongo.
   
 7. sister

  sister JF-Expert Member

  #7
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,029
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  pata picha huu utaratibu wa vitambulisho upelekwe hadi kwenye guest house na hotel.........upati chumba mpaka uonyeshe kitambulisho.
   
 8. Utamaduni

  Utamaduni JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 1,198
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Divert, Kurupuka Government at Work!
   
Loading...