Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 2,786
- 7,567
Wakuu,
Machi 7 Amos Makalla alisema CCM kwenye kikao cha ndani ilifanya marekebisho makubwa mawili katika mchakato wa uteuzi. Kwanza, kutakuwa na uchujaji wa wagombea kabla ya kura za maoni, tofauti na awali ambapo jina moja lilikuwa likirudishwa moja kwa moja. Pili, hakuna mgombea atakayepita bila kupingwa ndani ya chama na kisha kushinda bila upinzani nje.
"Hapo awali, mtu alichukua fomu na jina lake likarudishwa moja kwa moja, lakini sasa kutakuwa na mchujo wa awali. Majina matatu yatachujwa na kupigiwa kura za 'ndiyo' na 'hapana', hivyo hakuna anayepita bila kupingwa," alisema Makalla.
Hii ni tofauti na ilivyokuwa inafanyika awala ambapo wagombea wengine hata zaidi za 30 walishiriki moja kwa moja kwenye kura za maoni za wajumbe!
March 16 Makamu Mwenyekiti CCM Wassira alitoa msisitizo juu ya hili akiwa anahutubia wananchi Tunduma Machi 15, 2025 - Pre GE2025 - Wasira: Kura za maoni CCM mwaka huu majina ni matatu tu
April 10, CCM ilitaganza ratiba ya mchakato kwa wagombea ubunge na udiwani ambapo zoezi hilo lilitarajiwa kuanza tarehe 1 Mei, 2025, saa 2:00 asubuhi na kumalizika tarehe 15 Mei, 2025, saa 10:00 jioni, pamoja na mchakato mzima kwenye zoezi hilo - Pre GE2025 - CCM yatangaza kuanza kwa mchakato wa uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi Mkuu 2025.
Kutokana na ratiba hiyo Aprili 15, 2025 kuliibuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya wabunge wakisema kufanya hivyo kutawaondolea umakini wakati wa bunge la bajeti likiendelea akili ikiwa inawaza majimbo na kuchukua fomu - Pre GE2025 - Wabunge wa CCM walalamikia mchakato wa uchukuaji fomu kuanza mapema kabla ya Bunge kuvunjwa
Usiku wa kuamkia Machi 16, 2025 CCM walifanya mabadiliko ya mchakato huo ambapo badala ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kuwa siku 15 sasa imekuwa siku 5 pekee yaani kuanzia Juni 28, mpaka Julai 2, 2025, zoezi likitarajiwa kuanza siku 1 baada ya Rais kuvunja bunge.
Je, hii inamaanisha nini?
Kwanza, kamati ya roho mbaya inayokata majina na kupata yale matatu imekuwa na watu wachache inayoongozwa na Rais. Hii inamaanisha kama ni kuchechemua basi wa kuwafata ni Rais na wale wengine wanaoweza kumlainisha Rais, na hili tumeshaanza kuliona. Sasa hivi kila mtu Rais Samia hiki, mama kanipa kile, mama yupo kama malaika, hakuna mwingine kama mama, pamoja na kusifia wale woteee ambao wapo kwenye timu. Mkifuatilia vikao vya bunge wakati huu mtashuhudia haya. Yaani mtu anatumia dk 7 nzima kuwashukuru wale wotee ambao wapo kwenye kamati!
Pili, inakuwa ni njia ya kuwaengua wale wote wanaoonekana ni kidomo domo kwa serikali, wale ambao wanatia ugumu na kukaanga wafuasi wa mama, wale ambao kwa uwazi kabisa wameonesha kuchukukizwa na uchawa kwa mama, wale ambao walikuna kichwa wakati Samia anapitishwa kuwa mgombea kwa uchaguzi wa 2025

. Hapa cha kuwaokoa labda wananchi wakinukishe kukataa waliopitishwa maana kwenye chama kila mtu saiviakitaka kugoma tu anaambiwa unaona kilichompata Malisa? Sasa wewe neng'eneka.
Kwa upande mwingine inaonekana kama namna ya kupunguza rushwa kwa wajumbe, kwa kuwa mchakakato unapitia mchujo kwanza ndio uende kwa wajumbe na kisha watatu pekee kupitishwa basi vurugu za wajumbe zitapungua. Pia mchakato unafanyika mepema tu baada ya bunge kuvunjwa hii ikimaanisha pesa za kustaafu zinakuwa hazijatoka labda mtu awe amesave au watumie miradi ya pembeni, jambo ambalo hatutegemei wote wawe vizuri hapa. Lakini je, mchakato huo utapunguza kweli rushwa au rushwa ndio itahamia kule juu, atakayepanda dau sana ndio atakayepata 'zawadi'? Amna mwenye amekuwa loyal kwa mama toka day one ndio mwenye ataulamba?
Lakini kwa jicho jingine watu wataanza kuchafuana mapema kabisa ili kupunguza ushindani, yaani itakuwa muda wa kushuhudia makaburi yakifukuliwa na skendo za nyuma kuibuliwa ili amchafue kila anayemhisi anaweza kumpita mradi yeye apite, na kwa extreme case ni kurestishana in peace hata kwa kutumia waganga kuondoa wote watakauwa wanamuwekea kauzibe mtu. Hivyo mbali na skendo huu utakuwa ni muda wa waganga na viongozi wa dini kuneemeka na kutumika vizuri!
Je, unadhani hali itakuwaje huko mbele? Mabadiliko hayo yamefanywa kwa faida ya nani hasa?
Machi 7 Amos Makalla alisema CCM kwenye kikao cha ndani ilifanya marekebisho makubwa mawili katika mchakato wa uteuzi. Kwanza, kutakuwa na uchujaji wa wagombea kabla ya kura za maoni, tofauti na awali ambapo jina moja lilikuwa likirudishwa moja kwa moja. Pili, hakuna mgombea atakayepita bila kupingwa ndani ya chama na kisha kushinda bila upinzani nje.
"Hapo awali, mtu alichukua fomu na jina lake likarudishwa moja kwa moja, lakini sasa kutakuwa na mchujo wa awali. Majina matatu yatachujwa na kupigiwa kura za 'ndiyo' na 'hapana', hivyo hakuna anayepita bila kupingwa," alisema Makalla.
Hii ni tofauti na ilivyokuwa inafanyika awala ambapo wagombea wengine hata zaidi za 30 walishiriki moja kwa moja kwenye kura za maoni za wajumbe!
March 16 Makamu Mwenyekiti CCM Wassira alitoa msisitizo juu ya hili akiwa anahutubia wananchi Tunduma Machi 15, 2025 - Pre GE2025 - Wasira: Kura za maoni CCM mwaka huu majina ni matatu tu
April 10, CCM ilitaganza ratiba ya mchakato kwa wagombea ubunge na udiwani ambapo zoezi hilo lilitarajiwa kuanza tarehe 1 Mei, 2025, saa 2:00 asubuhi na kumalizika tarehe 15 Mei, 2025, saa 10:00 jioni, pamoja na mchakato mzima kwenye zoezi hilo - Pre GE2025 - CCM yatangaza kuanza kwa mchakato wa uteuzi wa Wagombea wa Uchaguzi Mkuu 2025.
Kutokana na ratiba hiyo Aprili 15, 2025 kuliibuka malalamiko kutoka kwa baadhi ya wabunge wakisema kufanya hivyo kutawaondolea umakini wakati wa bunge la bajeti likiendelea akili ikiwa inawaza majimbo na kuchukua fomu - Pre GE2025 - Wabunge wa CCM walalamikia mchakato wa uchukuaji fomu kuanza mapema kabla ya Bunge kuvunjwa
Usiku wa kuamkia Machi 16, 2025 CCM walifanya mabadiliko ya mchakato huo ambapo badala ya zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kuwa siku 15 sasa imekuwa siku 5 pekee yaani kuanzia Juni 28, mpaka Julai 2, 2025, zoezi likitarajiwa kuanza siku 1 baada ya Rais kuvunja bunge.
Je, hii inamaanisha nini?
Kwanza, kamati ya roho mbaya inayokata majina na kupata yale matatu imekuwa na watu wachache inayoongozwa na Rais. Hii inamaanisha kama ni kuchechemua basi wa kuwafata ni Rais na wale wengine wanaoweza kumlainisha Rais, na hili tumeshaanza kuliona. Sasa hivi kila mtu Rais Samia hiki, mama kanipa kile, mama yupo kama malaika, hakuna mwingine kama mama, pamoja na kusifia wale woteee ambao wapo kwenye timu. Mkifuatilia vikao vya bunge wakati huu mtashuhudia haya. Yaani mtu anatumia dk 7 nzima kuwashukuru wale wotee ambao wapo kwenye kamati!
Pili, inakuwa ni njia ya kuwaengua wale wote wanaoonekana ni kidomo domo kwa serikali, wale ambao wanatia ugumu na kukaanga wafuasi wa mama, wale ambao kwa uwazi kabisa wameonesha kuchukukizwa na uchawa kwa mama, wale ambao walikuna kichwa wakati Samia anapitishwa kuwa mgombea kwa uchaguzi wa 2025

. Hapa cha kuwaokoa labda wananchi wakinukishe kukataa waliopitishwa maana kwenye chama kila mtu saiviakitaka kugoma tu anaambiwa unaona kilichompata Malisa? Sasa wewe neng'eneka.Kwa upande mwingine inaonekana kama namna ya kupunguza rushwa kwa wajumbe, kwa kuwa mchakakato unapitia mchujo kwanza ndio uende kwa wajumbe na kisha watatu pekee kupitishwa basi vurugu za wajumbe zitapungua. Pia mchakato unafanyika mepema tu baada ya bunge kuvunjwa hii ikimaanisha pesa za kustaafu zinakuwa hazijatoka labda mtu awe amesave au watumie miradi ya pembeni, jambo ambalo hatutegemei wote wawe vizuri hapa. Lakini je, mchakato huo utapunguza kweli rushwa au rushwa ndio itahamia kule juu, atakayepanda dau sana ndio atakayepata 'zawadi'? Amna mwenye amekuwa loyal kwa mama toka day one ndio mwenye ataulamba?