Utapiamlo unaathiri kujifunza kwa watoto mashuleni?

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
250
Utapiamlo ni miongoni mwa changamoto kubwa inayoikabili Tanzania. Kati ya mwaka 2000 na 2010, zaidi ya watoto 600,000 wenye umri chini ya miaka 5 wanakisiwa kufa kwa kukosa lishe ya kutosha. Takwimu zinaonesha pia 60% ya watoto wa maeneo Mikoa yenye kiwango kikubwa cha uzalishaji wa chakula nchini ikiwemo Iringa na Kagera ndiyo inayoongoza kwa kiwango cha juu cha watoto wenye utapiamlo na udumavu katika umri wa chini ya miaka 5.

Taasisi ya Twaweza imefanya utafiti unaolenga kuonesha uhusiano kati ya utapiamlo na matokeo ya kujifunza uliofanywa mwaka 2015 kati ya mwezi Oktoba na Desemba katika kaya zaidi ya 60,000.

Ripoti ya utafiti huo itazinduliwa siku ya Alhamisi tarehe 22 Desemba 2016 kuanzia saa 8:00 hadi 10:00 mchana katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), School of Education kwenye semina ya JiElimishe iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Twaweza.
 
balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,025
2,000
Hapa lazima waje na pendekezo la kutoa uji wa lishe kwa madarasa ya awali kwenye shule zote za msing za umma nchini.
Hili tatizo ni kubwa na kiukwel linaadhiri ufundishaji na ujifunzaji kwa watoto. Sera mpya ya elimu (URT, 2014) inaeleza kuwa mtoto kuanzia miaka 5 anafaa kuanza darasa la awali hapo nauona uji wa lishe na sukari vikihitajika shuleni hivyo kuongeza gharama za uendeshaji wa shule zetu za msingi ukiachilia mbali ongezeko la uandikishaji watoto wa darasa awali plus uhaba wa walimu.
Guys kodi ilipwe tena sana tu elimu bure sio kisport-sport lazima tukaze. Tumeipenda wenyewe hii baba ni mbele kwa mbele. Uandikishaji mkubwa unaiambia serikali ajiri walimu wa msingi hata wajizungushe wataajiri tu fani ya ualimu ni bado marketable mpaka 2085 tena huu wa primary ndo wenyewe watu hawajui tu.
Suistainability ya ajira ya ualimu kwa nchi hizi zisizoendelea bado ni secured employment ever!!!
 
Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
1,439

Ila umasikini pia ni changamoto, maana mtoto atakunywa uji shuleni asubuhi lakini je uhakika wa kula baadae upo?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom