Suala la mahusiano ya kweli sasa limebaki katika maneno, kitendo ambacho kinasababisha cheni au mnyororo wa mtu mmoja kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja kushika kasi, na hili si mjini wala kijiji, wala haliko katika kabila fulani pekee.
Kwa hakika maisha ya leo unaweza kusema ni afadhali ya jana na hii ni kutokana na upendo kutoweka miongoni mwa jamii mbalimbali, na kujikuta ukiwa na upendo wa maneno kama ambavyo wengi wamekuwa wakielezana na kudanganyana kuwa nakupenda sana,nikinywa maji nakuona kwenye glas,tena nakupenda pekee yako.
Majina ya kitapeli mara baby mara honey mara hubby mara sweet n.k. kumbe kuna zaidi ya kumi wana ambiwa maneno kama hayo.
UTAPELI WA MAPENZI UMESHAMIRI KADRI SIKU ZINAVYOKWENDA KATIKA ULEMWENGU WA LEO!!!
Kuwa mjanja!