Katika kusubiria muda wa basi langu kuondoka nikaona nitembee kutafuta ngalau gazeti. Lahaula nikafika ktk kibanda fulani ivi mbele ya ofisi za shabibi kuelekea stand ya daladala.
Nikakuta watu wengi na kuna kama kibanda fulani cha kuuza vifaa kama tv, pikipik chakavu ivi. Kusimama nione, nikapewa CD ambayo wakaniambia ni matangazo ya kampuni fulani. Wakati nikitafari hayo, nikapewa namba kama za kucheza bahati nasibu.
Kufupisha simlizi, nikashinda pikipiki ya thaman 2, 000, 000 ambayo ni nzima ina card yake. Nikaulizwa kama naichukua au naiuza. Nikasema nauza kwani niko safarin. Nikaambiwa kuchangia kiasi cha 175, 000 ili kuipewa pikipiki au kupewa 2, 000, 000. Nikakataa nakuondoka. Sikujua ingétokea nini maana nilikuwa haraka kidogo.
Nadhani hii ni aina mpya ya utapeli au aliyekutana nayo atujuze ili tuwe salama.