Utapeli madhara yake na njia ya kuepuka

Utapeli madhara yake na njia ya kuepuka

Nebukadreza

Member
Joined
Dec 31, 2007
Posts
24
Reaction score
50
Utapeli ni janga ambalo limeumiza na linaendelea kuumiza watu wengi sana katika jamii. waathirika wa utapeli ni watu wa kada, jinsia na wazifa tofauti katika jamii bila kujali uwezo wa kiuchumi, elimu ,cheo au nafasi zao. Baati mbaya sana watu wengi wanaotapeliwa ni wa chache sana wanao weza kuweka wazi kwa sababu ya kuona aibu. miongoni mwa watu ninao wajua wamewahi kutapeliwa ni mabalozi, mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wafanyabiashara na watu wa kawaida. kama ungebaatika kujua kiwango cha fedha au mali walizotapeliwa watu ingekushangaza sana. matapeli wanambinu za kila aina hata sasa hivi ninavyoandika hapa kuna watu wanatapeliwa. lakini yote kwa yote chanzo cha utapeli ni vitu vitatu. Japo kuna utapeli wa kichawi lakini mpaka ww utoe nafasi
1. Tamaa .
2. Uzembe.
3. Uchoyo .
Binadamu ameumbiwa tamaa, huwa hariziki na hata kama akipata haamini kama amepata anataka apate zaidi. na huo ndio mlango wa kuingilia matapeli. fikiria mtu ana makazi ana biashara watoto wote amesomesha wanajitegemea na wanamsaidia lakini anataka dili ya mamilioni kwa njia ya mkato hapo lazima upigwe.
Binadamu ameumbiwa uzembe, kila kitu kina utaratibu, lakini unapotaka kufanya kitu kwa njia za panya na mtu anakuambia hiyo ni siri na wewe una fanya siri ili ule peke yako mwisho wa siku lazima upigwe.
Binadamu ameumbiwa
uchoyo, kitu chochote unapoaminishwa ukifanye siri lengo ni kuwa usipate muda wa kushauriwa na kwa kuwa roho ya uchoyo ina kuandama mwisho wa siku lazima upigwe.
Utaratibu wa maisha na mpango wa mungu huwezi kula bila kufanya kazi, hakuna kitu cha urahisi wala cha bure. bure ni ghali waswahili wanasema.
Hakuna siri ya watu wawili hiyo siri lazim itakuwa ni haramu.
Hakuna mtu yyt anayekupenda toka kusikojulikana, akitokea huyo anaajenda ya siri.


Ongezea mengine unayojua kuhusu waliotapeliwa
 
Watu wana utajiri wa kutisha kutokana na utapeli...
Muda mwingine wanashirikiana mpaka na polisi..

Sent using Nokia Torch 2108
 
Back
Top Bottom