Yaani mkuu haya matatizo ni mengi sana, cha msingi wakati wa kununua kitu kikishakuwa ni cha mtu mwingine hata kama yuko ulaya ni lazima uamuru aje hapa mwenyewe. Na kama hataweza basi angalao wakati wa mauziano chukua video, mchukue jamaa tu wako simple hata kwa laki mbili anakutolea DVD yenye masuali ya msingi ambapo utakuwa pia unawahoji hao viongozi wa serikali za mtaa. Nina hakika kama kuna ka uongo utaona wakikimbia kuhojiwa tu. Pia kama ni sehemu mtu alinunua mwambie akupe original karatasi ya kununulia eneo husika na ikiwezekana akupeleke kwa muuzaji kama atapatikana. Picha usisahamu mkubwa wangu, ziwekwe. Sema na viranja wakubwa wako Wizara ya Ardhi na Manispaa zetu hasa kama ni eneo muhimu au niseme liko maeneo mazuri.