VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Serikali ya awamu ya tano,chini ya Rais Magufuli,sasa imekuwa kama Jumba la Bigbrother. Kila juma la kazi,kuna mtumishi asiye mbishi anatumbuliwa,yaani kuachishwa kazi. Watumishi sasa hawana amani. Wanafanya kazi,si kwa weledi tena,ila kwa woga na mashaka.
Kila mtumishi anafanya kazi kwa woga unaompelekea kuwa mchonganishi na wa kuwasukumia wengine 'jumba bovu'. Watumishi sasa wanalazimika kujipendekeza hata kwa kuumiza ili wabaki salama. Serikali ya kuchongea na kuchongewa kwa ajili ya kutumbuliwa. Bigbrother.
Baada ya Kabwe,Simba na Kairuki kuaga kwenye Jumba la Bigbrother la awamu ya tano,watumishi wengine wanaendelea kupigiwa kura za ima kutoka au kubaki. Rais anapaswa kuwa makini na taarifa za majipu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam