youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Kuna rafiki yangu mmoja ambaye nilikuwa namheshimu na kumtumia kama mshauri wangu, lakini juzi kati amefanya kitendo ambacho kimenifanya nimuone hafai.
Heshima yangu nilikuwa nampa kwa kuwa alikuwa ameweza kuwa makini katika kuchagua mwanamke wa kuoa, na si hilo tu bali hata ndoa yake ilikuwa ni mfano kwa wengine kwani wameweza kuishi miaka zaidi ya mitatu ndani ya ndoa bila kuwa na ugomvi wa aina yoyote ile.
Chakushangaza eti juzi ilikuwa kama utani tu, yeye ni shabiki wa Yanga, sasa akamuuliza mkewe, "hivi mke wangu, wewe ni shabiki wa timu gani hapa Tanzania." mke akasema "mimi ni shabiki wa Simba",
Mmewe huku akionyesha sura ya kukasirika akamwambia "naomba ubebe kila kilicho chako uende kwenu isipokuwa wanangu tu."tukajua utani lakini mpaka hivi sasa wameshatengana mke yuko kwao na jamaa ndo amekomaa anasema hamtaki tena.