Utamu wa Penzi la Anko, siambiwi, sisikii (Sehemu ya Kwanza)

Utamu wa Penzi la Anko, siambiwi, sisikii (Sehemu ya Kwanza)

Ambakucha

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2019
Posts
403
Reaction score
676
Mtunzi Prince Oscar.

"We Doreen," mama aliniita kwa sauti ya ukali. Sikutegemea kumkuta yuko macho muda huo japokuwa alikuwa chumbani kwake. Ilikuwa saa nne usiku. Kwa kawaida mama ikishafika saa mbili usiku, siku nyingi yupo kitandani anaota ndoto anazozijua mwenyewe.

"Abee mama," niliitika huku nikitega sikio kusikia kichambo changu.
"Unatoka wapi?"
"Natoka kwenye bathidei ya Eliza mama."
"Ulimuaga nani?"

Yaani mama angu mimi hajawahi kuwa na maneno au maswali ya kufafanua sana. Ni shoti shoti tu. Angekuwa mama 'ako wewe si ajabu angekuuliza; unatoka wapi saa hizi? Au angeuliza ulimuaga nani wakati unaondoka kwamba unakwenda kwenye bathidei?

"Sikumuaga mtu mama," nilimjibu.

"Hongera sana kwa sababu humu ndani sasa ma mama tuko wawili."
"Hapana mama."

"Na huyo Eliza ulimfanyia bethidei bila yeye mwenyewe kuwepo?"
"Alikuwepo mama. Si ndiyo mwenye bathidei, kwa nini asiwepo?"

"Sasa mbona ametoka hapa kukuulizia muda si mrefu? Na akasema anakwenda msibani Kijiji cha Mgandini!"
Uso ulinishuka mwenzenu. Mashavu yalienda chini kama ninaye kunywa maji ya mti wa mwarobaini. Ukweli ni kwamba, sikwenda kwenye bathidei wala harusini bali nilikuwa kwa boifrendi wangu, Tom.

Tom ni mvulana tuliyependana sana ila tatizo moja alikuwa anataka kunitoa usichana wangu. Na mimi nilikuwa sikubali. Nilishajiwekea malengo kwamba, mwanaume atakayenioa ndiye atakayenitoa usichana wangu.

Sasa siku hiyo nilikuwa geto kwa Tom tukikukurushana. Yeye anataka, mimi sitaki.
Alifikia hatua akafunga mlango na kuchomoa funguo akidai nimpe kwanza anitoe usichana ndipo aniachie nirudi nyumbani. Lakini sikukubali. Nilibana miguu.

**************
Kwa hiyo, nilikosa jibu la kumpa mama. Lazima alijua nimetoka kwa wavulana na wameshanivua sketi. "Hiyo tabia yako uliyoianza Doreen iko siku utabeba mimba isiyokuwa na baba hapahapa nyumbani. Kwa hiyo jiandae na mahali pa kwenda kukaa," mama alinipa picha ya baadaye mapema ili nijue. Nisije nikamlaumu.

"Mama siwezi kupata mimba mimi," nilimjibu.
"Kwa sababu wewe ni mkamilifu sana?"

******************
Kifupi mama hakujua kama sipo chumbani kwangu. Ila alipokuja Eliza kuniulizia ndo ikajulikana kuwa, yaliyomo yamo hata kama hayana mdomo. Kwa hiyo baada ya Eliza kuondoka, muda wote alikuwa macho akinisubiri nirudi ili anipake rangi ninayoistahili.
******************
Baada ya wiki moja tangu kutokea kwa tukio lile, siku hiyo mama aliniambia natakiwa kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusoma sekondari ya binafsi. Alisema Dar nitapokelewa na anko Jailos na nitaishi nyumbani kwake. Nilijua mama alichukua uamuzi huo baada ya kuamini matendo yangu yamekuwa ya hovyo pale kijijini. Akajua nitaharibikiwa na mimba juu nikiwa nyumbani.

"Mama umeongea naye lakini huyo anko Jailos?"
"Unadhani nakurupuka kama wewe?"

"Sawa mama. Nitakwenda." "Ujiandae. Sitaki visingizio." "Sawa mama."
"Na ukienda sitaki kukuona umerudi cha likizo wala sikukuu. Labda kuwe na msiba. Tena niwe mimekufa mimi." Mama alikerwa na tabia yangu ya vivulanavulana.

Maana si mara moja kunigundua narudi muda mbovu. Na si ajabu alimwambia na anko kwamba nimeanza mahusiano wakati kumbe mwenzao wala, natunza usichana wangu.

Basi, siku ya safari ilifika, nikabeba nguo zangu kwenye begi la mgongoni, huyoo! Dar kwa anko Jailos.
Alikuja kunipokea stendi tukaenda nyumbani kwake, Tabata.

Nilioneshwa chumba changu cha kulala, bafu, jiko, stoo na vitu vingine vya nyumbani. Ilinichukua wiki moja tu, nilianza kidato cha kwanza kwenye shule moja ya sekondari.

Nilisoma vizuri hadi nikafika kidato cha pili. Nilikuwa nikipata matokeo mazuri maana nilijua nimekuja Dar kusoma na kwa sababu muda mwingi usia wa mama ulinijia kichwani mwangu. Nilipofika kidato cha tatu, nikiwa na umri wa miaka kumi na tisa, nilivunja ungo.

Wengine wanasema nilichelewa. Lakini mimi ninachojua ndo' ilikuwa wakati wangu. Sikuchelewa wala sikuwahi. Ila tofauti niliyoiona ni kwamba mwili wangu uliingia katika mabadiliko makubwa.

Nilianza kunawiri na kupendeza. Kila sehemu ya mwili wangu ilibeba jukumu lake.

Chakula cha mtoto kilisimama vizuri msimamo wake, watu waliuita saa sita mchana. Nyuma kulichomoza inavyotakiwa.

Vibastola navyo vilijitutumua ili kulinda viungo vingine kama sura, miguu, kiuno na kifua visishambuliwe kirahisi. Baadhi ya wanaume walianza kunimezea mate waziwazi hata wale ambao zamani waliniona mimi ni mchafukoge. Sasa siku moja nilipotoka shule, nilimkuta anko Jailos akijiandaa kutoka na gari. Sijui alikuwa akielekea wapi! Nilimsalimia kama ilivyo kawaida yangu.

"Shikamoo anko." Nilinesa kidogo kama napiga magoti ili kuashiria heshima na adabu kwa mtu aliyenizidi umri na pia ni mjomba 'angu.

Lakini anko aliitikia shikamoo yangu huku akiniangalia kwa macho yenye jambo fulani kuhusu mimi. Hilo jambo, liwe baya, liwe zuri.

Lakini ni jambo fulani kunihusu mimi Doreen.

Nilihisi kuna zaidi ya tatizo, haikuwa kawaida yake kuniangalia kwa macho ya vile hata kidogo.
Nilimwogopa sana anko siku hiyo kiasi cha kuhisi afadhali nisingekuja kusoma Dar. Moyoni nilisema nafuu ningebaki kwetu Morogoro nikaendelea kula nauli za akina Tom.

Lakini nilijiuliza kama nina kosa nitakimbilia wapi maana ndani ya nyumba tulikuwa tukiishi wawili tu. Mimi na yeye. Msichana wa kazi alishaondoka kwa kutoroka.

**************
Kifupi, anko Jailos alitengana na mke wake miaka minne nyuma. Sababu ya kutengana mimi sikujaliwa kuifahamu kwa vile wakati wanapishana lugha nilikuwa niko nyumbani, Morogoro nasoma shule ya msingi.
Baada ya kumaliza darasa la saba, sikuchaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari. Mwaka mmoja baadaye ndiyo akanichukua anko Jailos. Nilikuwa na miaka kumi na sita tu.

Yeye na mama yangu mzazi ni toka n'toke. Mkubwa mama. Kwa hiyo anko Jailos anaweza hata kupokea mahari yangu bila kipingamizi. Mama yangu ndiye aliyemuomba anko Jailos kunichukua mimi kuja kusoma hapa Dar es Salaam lengo ni kuniandaa na maisha yangu ya mbele na kuniepusha na mimba zisizotarajiwa.
Kigezo alichotumia mama ni kwamba, kule Morogoro naweza kuishia kwenye umalaya tu kama Eliza na mwenzake, Swaumu.

Kufika Dar, anko alinitafutia hiyo sekondari ambapo nilianza kidato cha kwanza nikijichanganya na 'mabesti luza' wengine wa shule za msingi. Ni shule iliyosifika kwa walimu wazuri japokuwa walimu haohao, hususan wa kiume walisifika pia kwa kucheza 'rigwaride' na wanafunzi wa kike. Hiyo simulizi niliikuta palepale shuleni. Kwa hiyo mimi haikunipa wasiwasi wala hofu kwani sikusikia kuwa walimu hao wanabaka. Ina maana ni maeleweno. Mimi nilijiambia nitakuwa sielewani nao. Tatizo liko wapi! Si sielewani nao tu. Basi, awali maisha yetu nyumbani na anko Jailos yalikuwa mazuri sana. Nyumba nzuri. Ina geti.

Anko alikuwa na gari na mlinzi wa getini ambaye baadaye alimtimua kwa sababu ya kulewa usiku akiwa kazini japokuwa muda mzuri wa kulewa pombe ni usiku.

************

"Sasa hili tatizo limetokea wapi, Doreen mimi," nilijiuliza. “Doreen,” anko aliniita kwa sauti iliyojaa utulivu wa hali ya juu baada ya kumaliza kuniangalia kwa yale macho ya saa zile. "Abee anko."
“Unajua kitu kilichokuleta hapa Dar es Salaam?”

“Nakijua anko. Nakijua," nilimjibu huku nikichekacheka kwa aibu kwani niliamini zaidi ya masomo sina kingine nilichokijua. Na sikujua yeye anazungumzia kitu gani. Hivyo nilijaribu kubeti. Mimi na anko Jailos hatukuwa na tabia ya kutaniana kama walivyo maanko wengine wa kiume na maanko zao wa kike. “Ni nini?” aliniuliza anko huku akiwa amekunja sura au uso kuashiria kwamba hanitanii kwa hilo alilokuwa akiliongea wakati huo.
“Nimekuja kusoma anko.”

“Sasa unasoma?” anko alinichapa swali ambalo katu sikulitarajia achilia mbali kulitegemea.
Moyoni nilisema mh! Makubwa! Kabla sijamjibu nilijiuliza anko amegundua nini? Nilipitia nyendo zangu zote za wiki hiyo hata nilipotongozwa na rafiki yake, Mudy.

"Lakini kama Mudy ndiyo amemwambia mimi sijatulia, mbona nilimkatalia. Ningemkubalia hapo sawa," niliwaza. Halafu nikamrudia anko:

“Mbona nasoma anko au hauoni?” nilimpa jibu kama la kumsuta. Nilitamani niende chumbani nikamletee begi langu la shule aone kazi zangu.

“Zaidi ya kusoma shuleni mnafundishwa nini kingine?” Loo! hili nalo nililiona ni lingine aisee. Kwa hiyo beting yangu mkeka ulichanika! Yaani anko sikumuelewa hata kidogo. Nilijua swali lake lilikuwa na maana, halikutokea vivi hivi tu kwamba aliamua kusema. La! Nilikataa.

“Anko, kwa nini umeniuliza hivyo? Kwani kuna nini umesikia? Niambie nijue anko ili kama nimekosa mahali nijirekebishe. Maana mimi naye ni binadamu,” na mimi nilimuuliza. Si unatujua Wabongo tena. Swali mwenzake ni swali.

“Wewe una uwezo wa kuniuliza bila kunijibu?” anko alinishtukia kwamba nilitaka kumchunguza bila mwenyewe kujua. Nilimwangalia kwa macho ya tofauti na siku nyingine. Alitisha sana siku hiyo kuliko siku nyingine zozote zile tangu nilipoanza kumfahamu. Hata alipokuwa akija nyumbani. “Tunafundishwa masomo,” nilimjibu huku nikisikilizia jibu lake.

“Mnafundishwa masomo tu? Hakuna lingine, si ndiyo ee?" "Ndiyo anko. Kwani kuna nini kingine umeambiwa tunafundishwa?" Hili swali nilimuuliza kwa kulipindisha tu. Lakini swali orijino nililotaka kumuuliza lilikuwa hivi, "anko we si ndiyo ulinitafutia ile shule, 'sasa kama kuna kingine tunafundishwa siyo kizuri kwa nini ulinipeleka pale?"

“Sawa. Lakini mbona kama naona wewe unajua na mambo mengine mengi?” anko aliniambia huku bado macho ameyakaza kwangu.

“Yapi mengine ninayoyajua anko?” nilimuuliza huku nikijiangalia nilivyo.
“Jiangelie sana nakwambia, tena jiangalie,” alisema huku akiondoka kwenda chumbani kwake.

Itakuwa ikiwajia kila siku.
Weka like ikiipenda. Maoni/Ushauri nachukua.

Hadithi yote ina maneno 26,723. Unaweza kuipata yoote kwa Tsh. 1,500/= tu. 0785 990097.
 
Hongera kwa Simulizi nzuri mkuu, Japo sijasoma lakini inaonekana ni simulizi nzuri, kuanzia Jina la Hadithi, upangiliaji wa Simulizi na Uandishi kwa Ujumla.

Usikatishwe Tamaa na wanao,kukatisha Tamaa Usirudi Nyuma, Uliahidi kuleta vipande vya simulizi hii hapa Jf Kila siku lakini hujaleta.

Huenda hii simulizi Imesomwa na watu zaidi ya Mia mbili 200 waliofungua uzi ni watu 302 hadi sasa.

Binafsi si msomaji sana wa story.
LAbda iwe weekend na nikute simulizi iliyo kamili.

All the best mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom