Kama utamu upo kwenye sukari mbona vyengine ni vya chumvi nahuwa vitamu? Na kama utamu upo kwenye chakula mbona vyengine haviliwi na vitamu? Nakama utamu upo kwenye furaha saa nyengine mbona kwenye ugomvi panakuwa patamu? Hebu nambieni utamu upo wapi hasa?
Nipo pamoja nawe mkuu sina nia ya kukupinga ila raha mtu hajipi mwenyewe so utamu utakuwa upo kwa mwenzako au upo wapi hasa? Mana kidole kimoja hakivunji chawa na nazi haijikuni mwenyewe mpaka akuwepo mkunaji!
Mbona kuna vyengine vya chumvi? Kwa mfano kileja,biscut, maharage matamu kweli kweli tena wala hayatiwi sukari hapa mm nipo njia panda utamu uwe wowote unaoujua wewe ila sehemu yake maalum haswa mm bado sijaufaham