Utamtambuaje mwenye mapenzi ya kweli?????

Utamtambuaje mwenye mapenzi ya kweli?????

MR. ABLE

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
1,480
Reaction score
946
Nimeandika mada hii kutokana na watu wengi kushindwa kutofautisha kupendwa kweli na kutamaniwa. Wapo walioingia mkenge kwa neno hilo hasa walio wageni katika uwanja huu wa mahaba. Ukiambiwa unapendwa basi unachanganyikiwa na kusahau maneno matupu hayajengi nyumba.

Nina maana gani?

Watu wengi wamekuwa wakitumia neno hili kama mtego wa kumpata mtu, kwa kujifanya anakupenda sana na nahau nyingi za mapenzi ambazo zinaweza kukufanya masikio yako yazibe na kuona nani kama wewe.

Siku zote mtafutaji ana lugha tamu ya mapenzi na kabla ya kutamka lolote lazima atangulize nakupenda sana na kuongezea ajuavyo. Hii si mara moja watu kuingia mkenge inapotokea wanakutana na hali hiyo.

Lazima uelewe serikali ya mwili wako inakutegemea wewe, ukiipeleka vibaya lawama zitakuwa juu yako. Usiwe na papara ya kutoa uamuzi wa kukubali uambiwavyo unapendwa bila kufikiria kwa kina. Hakuna hata siku moja mtu anayekutaka kimapenzi akuambie anakuchukia.

Fikiri kabla ya kutenda na kuona kauli uliyopewa ina nia gani na wewe, kweli anakupenda au anataka kukuchezea na kukuacha.

Katika uchunguzi wangu nimegundua wengi hupima kwa masikio juu ya kile aambiwacho na si kufikiria nini hasa kilichomvutia aliyekutamkia maneno hayo. Japo kakutamkia anakupenda, ni vema ukafanya kadiri uwezavyo kupata muda kufikiria kwa kina kabla ya kutoa uamuzi wowote ambao unaweza kukufanya uwe na faida au hasara.

Neno nakupenda siyo mapenzi kamili, bali tabia ya mtu na kuonyesha kweli anakupenda kwa dhati. Akupendaye huwa hana haraka ya kufanya ngono, hufuata taratibu zote ili mradi kujenga uaminifu moyoni mwako.

Hii hutokana na kuwa na uhakika wewe ni wake, hana hofu ya kutanguliza ngono mbele katika uhusiano wenu wa kimapenzi. Ukiona umekutana na mtu anayetanguliza ngono baada ya neno nakupenda huyo hakupendi bali anakutamani.

Tumekuwa tunatumia neno nakupenda kama kiwakilishi cha ujumbe wa mapenzi na si penzi kamili.
Mapenzi ya kweli ni ya vitendo na si maneno, anayekupenda utamjua tu wala hajifichi. Atakuwa mpole, mwenye huruma, anayekujali, muaminifu na mtu aliye muwazi mwenye kukupa uhuru wa kumjua kwa undani ili kukuondoa wasiwasi.

Mapenzi mengi ya siku hizi yamekuwa ya usiri mkubwa yenye mipaka. Kama kweli anakupenda kwa nini akudanganye na akuwekee mipaka ya kumjua?
 
Umeandika kama unaishi miaka ya 80s. Unafikiri miaka ya sasa kuna upendo wa dhati? Kama unafikiri hivyo umekwisha! Siku hizi ni kutamaniana na maslahi tu hakuna zaidi.
 
Umeandika kama unaishi miaka ya 80s. Unafikiri miaka ya sasa kuna upendo wa dhati? Kama unafikiri hivyo umekwisha! Siku hizi ni kutamaniana na maslahi tu hakuna zaidi.

Bra-joe, sasa hivi mapenzi yamepungua na sio kufa kabisa kwa7bu watu wameshhindwa kuangalia moyo unasema nini na badala yake kuangalia mwili unasema nini.

Hii hufanya watu wengi kutokuwa na mapenzi ya dhati sababu ya kuendekeza tamaa za mwili hivyo mwishowe huzoea tabia hio na kuwa yakudumu na kushindwa kupenda tena bali kutamani tu.

Ila naamini watu wakitulia na kuusikiliza moyo wao kwa kile moyo unachosema tutaondokana na hii dhana ya kutamaniana kama KUKU.
 
Ukimpata kama ana mapenzi ya kweli na siyo tapeli utamtambua tu lakini siku hizi wenye mapenzi ya mafungu ya nyanya wako wengi sana. Atakupenda wewe 20% mwingine 25% na mwingine 10% na aliyebaki 45%.

Last edited by a moderator:
kwa maneno kwa vitendo na kwakutambua wajibu wake anacho takiwa kufanya nini ,hekma na busara navyo visibaki nyuma
 
funga siku arobaini bila kula wala kunywa utampata mwenye mapenzi ya dhati na kweli
 
Tumeamua kuacha mila na desturi zetu za ASILI na kuiga sio mila na desturi za wazungu bali kufuata tabia ya MAFUSKA wa kizungu wanavofanya.
 
Bra-joe, sasa hivi mapenzi yamepungua na sio kufa kabisa kwa7bu watu wameshhindwa kuangalia moyo unasema nini na badala yake kuangalia mwili unasema nini.

Hii hufanya watu wengi kutokuwa na mapenzi ya dhati sababu ya kuendekeza tamaa za mwili hivyo mwishowe huzoea tabia hio na kuwa yakudumu na kushindwa kupenda tena bali kutamani tu.

Ila naamini watu wakitulia na kuusikiliza moyo wao kwa kile moyo unachosema tutaondokana na hii dhana ya kutamaniana kama KUKU.

ndugu, ukiufuata moyo ndiyo utaumia sana ktk mapenzi, kwani unayempenda kwa dhati hakupendi hata kidogo na usiyempenda anakuganda kama gundi. Bora kufuata tamaa za mwili. Tafakari.
 
ndugu, ukiufuata moyo ndiyo utaumia sana ktk mapenzi, kwani unayempenda kwa dhati hakupendi hata kidogo na usiyempenda anakuganda kama gundi. Bora kufuata tamaa za mwili. Tafakari.

Bra-joe kwani mpaka sasa unaangalia mwili unasema nni badala yakuangalia moyo unasema nini????
 
Mapenzi ya kweli hayajifichi hata kidogo ko kwa mtu mwenye akil lazima utajua tu kama unadanganywa
 
kwakuomba na kufunga kwani mpenzi bora na mzuri hutoka kwa MUNGU.

upo sawa bt hii pia ni kipaji coz Mungu anaweza akakuonyesha lakini kwa ubishi na macho yako ya binadam ukabisha na kuuvaa mkenge
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom