Utamtambuaje mwanamke mwenye future kwako?

Utamtambuaje mwanamke mwenye future kwako?

Wadau nahitaji kufaham mwanamke mwenye malengo kwako niwa aina gani.
'Future'! Binadamu tuna maisha yenye mirengo mbalimbali tofauti tofauti.

Sasa hauwezi kuleta swali la mwanamke mwenye 'future' zako kwenye kadamnasi wakati 'future' zimetofautiana, 'future' unayoongelea wewe hapa ni 'future' gani?

Kuna wengine ni majizi, majambazi au matapeli, lakini wana wake zao.

Kuna watu hohehahe lakini wana wake zao pia!

Tongoza atakayekukubalia na kuonesha upendo, huyo ndiyo wa 'future' zako bila kujali 'future' zako hizo ni zipi.

Naye atakapokuja kugundua kuwa wewe nawe si wa 'future' zake atakukimbia, elewa hivyo.
 
....thamani ya mwenza iko machoni na moyoni mwako...Sali omba hekima na Mungu mpaji akufungue macho uone ubavu wako uliko...

..Vionjo vyako (kimwili/kimaongezi/kihisia/uvumilivu ect. ) juu ya mwenza wako haviwezi fanana na vya mwingine ....ushauri wa jamaa/marafiki ni asilimia 15% ya maisha yako na mwenza wako..
 
Na mtu wa kumuoa au kuolewa huwa anakuja tu pale unapokuwa na nia wala huwez jua na huyo ndo aliyekuwa kandaliwa kwajili yako
 
Acha wakati uamue yupi utaenda nae huko future,,, ukianza kuumiza kichwa mapema hutapata lolote.
 
Back
Top Bottom