Utamtambuaje mwanamke kama amekupenda?

Bacore

JF-Expert Member
Oct 20, 2017
222
228
Habari zenu wakuu,

Kama kichwa cha habari cha jieleza,

Kujua hisia za wanawake sisi wanaume huwa inaweza ikawa ni ngumu sana, tujaribu kubadalishana mawazo, nitajuaje kuwa wewe mwanamke umenipenda, hapa nazungunzia zile hatua za awali, hatua ambazo hatujafahamiana lakini tunaonana mara kwa mara, kama sehemu zenye mikusanyiko inayotufanya tukutane, labda ni kanisani, chuoni, barabarani nk.

Wanawake wengi wanaishia kuumia moyoni juu ya wale wanaowapenda, lakini ugumu ni pale wanaposhindwa kuwaambia wanaume hisia zao moja kwa moja, bali kuanza kutumia njia zingine za kufikisha azma yao, ili kutimiza matakwa yao ya kimapenzi dhidi ya watu wanaowapenda,

Sasa wewe mwanamke mimi ni mwanaume, ninajuaje kama kweli wewe mwanamke umenipenda ila umefikisha ujumbe wako kwa njia indirect, manake sisi wanaume inakuwa kazi kutambua haya moja kwa moja, unakuta mwanamke anajichekesha hata pasipo kuchekeshwa,au unafanya kitu na kutumia nguvu nyingi kufikisha ujumbe!

Ifikie mahala wanawake muanze kutuambia ukweli dhidi ya hisia zenu, ukipenda kijana mwambia kuwa umempenda i mean, umtongoze lakini kutumia nguvu nyingi kufikisha ujumbe inawaumiza sana wanawake walio wengi.

Karibuni tuchangie na tujifunza yale tusiyoyajua!
 
Back
Top Bottom