Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,440
- 38,437
Ni alasiri ya Ijumaa, mmeshindaje wanawema wa JF?
Angalia haya ili umtambue rafiki wa kweli:
uaminifu -
Uaminifu ni sifa ambayo ni lazima ionekane kwa mtu unaeamini km rfk yako. Huyu anakuwa ni mtu ambaye anayajua yako, na anayatunza ama kuifadhi kwa vile wewe umemuamini na kushare nae hayo uliopenda kushare nae. Asiwe muongo muongo, mbadilisha kauli, kwa kfp awe msema kweli!
uwelewa na ufahamu:
Kuwa na rafiki mzuri inahusisha na rfk mwenye ufahamu wa mahitaji yako na kutambua maadili yako, kinyume chake anakuwa ni mtu mjinga, na hataweza kufikiria yenu na kuyachambua kama marafiki kwa manufaa yenu wote, hapa anapoteza sifa ya rfk.
unyeti
awe anaguswa na yale masuala ambayo ww kama rfk umeamini ni nyeti na kwa unyeti ule, umemuona yy ni mtu stahiki kujua yale ambayo pengine mwanafamilia asingeweza kupewa, km hajali mambo nyeti baina yenu, mmmh, mtafutie msamiati mwingine, si rfk!
Furaha
Rfk mzuri ni yule ambaye anafurahi na wewe kpnd cha furaha na anahuzunika na wewe kipindi cha huzuni, anaenda mbali zaidi kwa kukutafutia furaha ama amani wkt ukiwa ktk majanga, tena kwa kutumia resources zake ikibidi! Kinyume chake, hapo huna rfk, kumbuka kwa muktadha huu, baadhi ya ndg huwa ni marafiki by natural law!
kusikiliza
Huwa tunapata marafiki kwa vile tunawasiliana, na tunawasiliana kwa vile tunasikilizana, tukishasikilizana tunafahamiana zile interests zetu, na hapo urafiki huchanua! kama rfk hakusikilizi basi hapo una mtu wa aina nyingine na sio rfk!
Mbeleko:
Rafiki mwema atakuwa mbeleko, ama wakati mwingine tunasema daraja! Si lazima awe hivo milele, lkn ktk historia ya urfk wenu lzm kuwe na sehemu ambayo ama wewe ama yeye, mmoja alikuwa mbeleko ama daraja kwa mwenzie! Kinyume cha hii, ni kuwa na rfk mzigo, na hii si lengo la urafiki!
ukarimu:
Rafiki mzuri ni wazi atakuwa na ukarimu katika maeneo muhimu km utu na tabia. Atakuwa na ukarimu ambao unatoa mwanya kwa rfk kufunguka na kuweza kutoa yale ya moyoni, na mwenzake akajua!
Nimejaribu kuchambua wapendwa, wakati mwingine si lzm rfk yako awe na sifa hz zt, na hasa kama urafiki wenu ni ule wa kimaslahi!