Utamshaurije huyu??

sakimbo

Member
Joined
Apr 1, 2015
Posts
10
Reaction score
1
Ni binti ambaye wazazi wake walishafarik kipindi kirefu kilichopita, ila wazaz wake enzi za uhai wao walikuwa hawaelewani hadi kufikia kuachana, baada ya mama yake kufarik binti alilelewa na bibi na wajomba wakamsomesha hadi kuhitimu elimu ya chuo kikuu bila kupata msaada wowote kutoka kwa ndugu wa upande wa baba, sasa amepata mchumba na anahitaji kuolewa,wajomba na bib hawataki binti huyo awahusishe ndugu wa upande wa baba yake kuhusu maswala yote ya harusi, lakin kwa upande mwingine ndugu na wazazi wa mchumba wake wanahitaji ndugu wa upande wa baba wa binti huyo was hi Riki sh we, tafadhali tunaomba ushauri wako kwa binti huyu.....
 
kukutana kwenye matukio kama sherehe na misiba kumamaliza mabifu
 
wamalize tu hizo tofauti zao......ili walikamilishe hili zoezi muhimu kwa binti....afu hayo mengine wayaendeleze baadae.......
 
Hakuna shida kuwashirikisha kwa kuwa wote wanahitajika ila vile anawajua hauitomsumbua kuishi nao
 
Yaliyopita si ndwele wagange yajayo,waweke tofauti zao pembeni waunganishe ushirikiano kufanikisha tukio la binti!
 
Mila & desturi za Kabila husika zinasemaje? Maana hizo ndizo jadi yetu na zinatoa muongozo kwa masuala tata kama haya. Mfano, kwa wasukuma mwanamke ukimtolea mahari basi mtoto akizaliwa ni wako na una haki zote na siku akiolewa (kama ni binti) basi mahari hiyo ni haki yako. Kama hujatoa mahari basi una wajibu wa kumtolea mahari mtoto wako. Ukiwa hujamtolea mahari mama wala mtoto basi mtoto si wako na huna haki yoyote juu yake. Kwa wayao & wamakua mtoto ni Mali ya mama na linapokuja suala la kuolewa kwa binti shughuli nzima husimamiwa na wajomba, hii ikawa ni Pamoja na kupatanisha mahari na kuitumia.
 
Yan umegusa palivyo binti ni msukuma na bibi anasema kuwa baba wa binti huyo hakutoa mahari kwa mama wa binti huyo hapo itakuaje tukirud kwenye mila na desturi?
 
Wakikutana yatakwisha tu, tena mahali kama misiba au sherehe, tofauti huo zinaishaga na kujikuta mnashirikiana.
 
Waambiwe tu ili kama wakiweza washiriki, ila wasishirikishwe jambo lolote, maana mzazi halisi hapo ni bibi.
Ndugu wa wanaume jifunzeni kutoingilia ugomvi wa watu waliozaa, maana mwisho wasiku inakuwa aibu yenu.
 
Yan umegusa palivyo binti ni msukuma na bibi anasema kuwa baba wa binti huyo hakutoa mahari kwa mama wa binti huyo hapo itakuaje tukirud kwenye mila na desturi?
Wajomba ndio wana haki ya kuchukua hiyo mahari sio kwa sababu walimsomesha bali kwa sababu baba wa mtoto hakutoa mahari. Lau angekuwa ametoa mahari ima kwa mama wa mtoto au kwa mtoto mwenyewe basi ndugu upande wa Baba wangekuwa na haki. Nyanya /bibi wa mtoto anasimamia mila & desturi muungeni mkono ktk hili.
 
Haya ni matokeo ya not being responsible to our families. Both men and women!!! Tuwe makini ukiamua kuzaa basi uamue kulea.
 
Mmmh pagumu hapo..mimi kama mimi ningefanya ila kwa shingo upande.Kwanini hao ndugu wamsuse mtoto wao? Hata kama wazazi waligombana,mtoto hahusiki wamefanya vibaya.
 

Sasa na utambulisho itakuaje?? Yan maanisha upande wa kijana anayetaka kuoa itakuwa vyema wazazi wake wakienda kujitambulisha upande wa baba wa binti huyo? Kisha kuja kujitambulisha tena kwa wajomba?? Naomba msaad wa Mawazo tafadhali
 
Hao waoji haeajaambiwa mtoto huyo kalelewa ujombani?????
 
dini zinawafanya watu wanachanganyikiwa... badala ya mtu kuona watu wanauliwa na wauuaji, anaona muislamu anauliwa au anaona mkristo anauliwa. watu wanahisi dini zina uhusiano mkubwa sana na wao kiasi kwamba wanaweza kuua kwa ajili ya dini. uuaji ni uuaji, ukatili ni ukatili, haijalishi umefanywa na nani, tunakumbatia imani za dini mpaka tunasahau sisi ni nani. nitafurahi saana pale watu watakapo funguka na kuacha na kujifunga na parasite-dini.
 
hapo bora ndoa isiwepo ila kujipendekeza kwa ndugu wasiokijali sio ishu kabisa...
la maana ni kuwaambia tu ukweli upande wa mchumba wake.....!!!!!
 
Sasa na utambulisho itakuaje?? Yan maanisha upande wa kijana anayetaka kuoa itakuwa vyema wazazi wake wakienda kujitambulisha upande wa baba wa binti huyo? Kisha kuja kujitambulisha tena kwa wajomba?? Naomba msaad wa Mawazo tafadhali
Nendeni mkajitambulishe upande wa Wajomba, hao ndio kila kitu kwa Sasa. Pengine kinachowashangaza ni kwa kuwa huo sio utamaduni wenu. Mkifanya mnavyotaka kufanya ni Sawa na "supu kuitia nazi". Mila na desturi zetu ziliwekwa ili kujibu maswali magumu na kusisitiza nidhamu kwa jamii na mtu mmoja mmoja.
 

Sawa nmekuelewa ila tatzo ni kwamba upande wa kijana wanasema mila na desturi zao hawawez kujitambulisha kwa wajomba lazima waende upande wa baba wa binti huyo kwanza wao ndio wawape ruhusa ya kwenda kujitambulisha kwa wajomba, na upande wa pili bibi hataki upande wa baba wahusishwe, itakuaje hapo sasa,??
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…