TAECOLTD
JF-Expert Member
- Mar 2, 2013
- 1,051
- 1,845
Enzi zile tulifundishwa heshima na adabu kwa wakubwa zetu popote pale na nimekua hadi leo na 30's ila kuna tatizo naliona linazidi kushika mizizi kwa hawa wadogo zetu
Kawaida huwa natumia huu usafiri wa mwendokasi (tuweke adha zake pembeni kwanza), kwa asilimia kubwa huwa napata siti labda kutokana na aina ya shule nilizosoma mjini miaka hiyo secondary kugombania, ila unakuta hawa watoto wa shule wasichana kwa wavulana wamekaa kwenye siti. Unakuta kuna watu wazima makamo hata ya babu zangu wamesimama kawaida huwa nawapisha siti wakae ila tatizo ni hawa watoto.
Unakuta wamejikausha kama hawaoni, wamekaa bila aibu tena mara zingine wanapiga story wenyewe kwa wenyewe bila haya usoni.
Je ni kwamba shule hawafundishwi tena kuhusu maadili na heshima kwa watu wazima? Au wazazi wamechangia kwa asilimia kubwa kuwatia viburi watoto hawa wawapo nyumbani? Mara kadhaa kwenye daladala nimeshuhudia wakina mama wakilipia nauli ya watu wazima watoto wao ili wakae kwenye siti ilihali watu wazima wamesimama je huku sio kuwaharibu watoto tangu wapo wadogo hadi wakikua?
Maadili yetu yapo wapi sasa hivi au ndio utandawazi unatuangamiza? Utasema ni hela zao acha wajinafasi ila je huko tunapoenda hali si ndio itakua mbaya sana kwa hawa watoto kimaadili?
Nadhani hii ni tatizo pia linapelekea taaluma za hawa watoto zinazidi kuporomoka sababu kama hawana heshima wala utii kwa wakubwa zao unadhani watakua serious ku catch up wanachopaswa kusoma na kufaulu?
Ni wapi tumepotezea maadili yetu ili tuweze kuyarekebisha? Tunapaswa kujichunguza upya