Utamaduni wa Usiri unatuletea vurugu Tanzania

Utamaduni wa Usiri unatuletea vurugu Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,836
Reaction score
15,627
Kama mnakumbuka vurugu za miezi michache iliyopita Mtwara Waziri mkuu alikwenda kuongea na wananchi wa Mtwara na kueleza mipango ya serikali ya maendeleo kwa kusini. Kwa mara ya kwanza wananchi wa kawaida walijua mipango ya serikali lakini vilevile hii imeonyesha tatizo kubwa tulio nalo Tanzania.

Watanzania na serikali kwa ujumla tuna utamaduni wa usiri kwa mambo ambayo hayatakiwi kuwa siri na uwazi kwa mambo ambayo yanatakiwa kuwa siri. Serikali kama ina nia nzuri ingechapisha sera zake zote kwa uwazi na kwa kiswahili na kuwapa wananchi na vyombo vya habari ili watu wajue kwamba serikali inafanya vitu na ni kwa nia njema. Hii itasadia mambo muhimu kama ifuatavyo (1) Itapunguza uvumi kwamba sera zote za serikali ni za kifisadi kitu ambacho ndiyo cha kwanza kwa wananchi wengi kwa sasa (2) Itapunguza wananchi kufikiria upendeleo wa mikoa (3) Italeta utamaduni wa kukosolewa kama sera si nzuri itakoselewa na serikali inaweza kubadilisha (4) Itaongeza uwekezaji kwasabau wawekezaji hawatasubiri kukutana na waziri au viongozi wa nchi kuelewa sera za uwekezaji hasa kwenye madini, gas, oil na kilimo. Sheria zao na mipango yote inatakiwa kuwekwa kwenye mtandao wa serikali ili kila mtu aweze kuona na kukosoa hakuna sababu ya siri kama kweli tunaitakia nchi yetu usalama. Bila uwazi fujo za wananchi hazitaisha na polisi pekee hawawezi kubadilisha fikra za wananchi na ushirikiano wa kimaendeleo hasa kama wananchi wana hisia za kuibiwa na mafisadi serikalini.Hivyo uwito wangu ni kwa serikali kabla hata ya kuweka mipango mizuri ni lazima waweke utamaduni wa uwazi kwani utamaduni wa siri ni adui mkubwa kuliko ufisadi.

Utamaduni wa uwazi vilevile uendane na utamaduni wa ukweli na wananchi ni lazima waambiwe ukweli ili waweze kubadika na kujiletea maendeo bila kufanya siri mfano.

. Kwenye magaidi wa dini: Ukweli ni kwamba magaidi wa kidini ni waislamu wenye siasa kali na wanapinga wasilamu wengine ambao wanajichanganya kwenye jamii, wakisto, pagani na watu wote wanaoamini tofauti na wenyewe. Arusha wamelipua kanisa lakini vilevile walimvamia kiongozi wa Bakwata ambaye ni mwislamu kama nakumbuka walimpiga risasi. Huu ni ukweli lakini serikali kudanganja na kutaka kumfanya kijana wa miaka kumi na nane (18) mwendesha bodaboda mkrito ndiye aliyelipua kanisa bila kuonyesha nia uwezo haiitasaidia kutatua tatizo hili. Tatizo hili halijaanza Arusha. Ukweli utasaidia badala ya kuweka siri kwani siri itaonyesha kama ni watu wengi wana wasapoti hawa magaidi au ni dini kwa dini lakini ukweli ni kwamba ni watu wachache.

. Elimu na maendeleo: Utamaduni unachangia kwenye maendelo na sehemu nyingi zenye maendeleo ni kwasabau zina elimu na kuna utamaduni wa elimu. Hivyo ni lazima tuseme hilo Mkoa wa Kilimanjaro na Arusha una shule nyingi kuliko zanzibar yote na wanafunzi wanafanya vizuri kuliko sehemu nyingine zenye rasilimali zaidi si kwasababu ya kusaidiwa na serikali au vyama vya siasa bali ni kwasabau ya utamaduni. Wamasai wengi hawako shule kwasababu ya utamaduni! ukienda Pwani watoto wa miaka 16 wanaolewa sasa watapata elimu lini? hivyo serikali na wananchi tuambiane ukweli kwani ndiyo siri kubwa ya maendeleo. Huwezi kuendelea kwa siri.
 
Huu kweli ni ushauri wa bure kwa watawala-lakini nahisi ni viburi au wao wanaishi TZ gani mambo yamebadilika hamna kutawala kwa propaganda zisizo na mashiko tena na ukiukwaji wa kutekeleza ahadi

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom