Utamaduni wa kuongea unaleta tija kwa taifa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utamaduni wa kuongea unaleta tija kwa taifa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Invarbrass, Jan 3, 2012.

 1. Invarbrass

  Invarbrass JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kuna kasumba inaanza kuota mizizi hapa nchini yakupenda kuongea kana kwamba kuongea ni dawa ya matatizo yote ya nchi yetu. Yaani inanichosha kweli kweli. Utakuta tukio fulani linatokea basi kesho yake kuanzia redio tv na kila atakayepata nafasi ataliongerea hilo. Mfano magufuli kapishana lugha na watu wakigamboni basi hatulali kila mtu kuanzia wabunge, redio, tv, vijiweni maofisini, kwenye daladala na bar ndo mjadala.

  Hivi tutajenga nchi kwa kukosoa kauli tu? hivi hii nchi kazi yetu kubwa ni kukuza mijadala? hivi muda tunaotumia kuongea hatupotezi muda wa kufanya kazi? kama magufuli kakosea ndo wote tuache kazi na kuongelea hilo?

  Matokeo yake tunaanza kuthamini kiongozi anayeongea sana badala ya yule anayetenda kazi. Utasikia mara ooh mbunge fulani kiboko anaongea huyo ni mzuri sana. Ndio maaana taifa hili polojo nyingi kuliko kazi.

  Ugonjwa huu umeenea hata kwa raia wa kawaida. Mtu akikaaa akaona kama watu hawamjui au wamemsahau vile anaibuka maelezo anapiga polojo ooh! taifa linaelekea kubaya, ooh! ufisadi unalitafuna taifa. leta suluhisho

  Hata viongozi wa dini wao ndio wataalam wa kurekebisha roho sasa kama jamii haina maadili( wizi, rushwa, ufisadi na takataka kibao) nani alaumiwe kama sio wao. Lakini utakuta nao kutwa kucha kwenye vyombo vya habari eti wanalalamika taifa linaenda kubaya.

  WITO: MCHANGO WA MALALAMIKO UMETOSHA SASA TUANZE KUCHANGIA MAENDELEO YA NCHI YETU KWA KILA MMMOJA KUTIMIZA WAJIBU WAKE. MVIVU TUTAMJUA NA MZURI TUTAMJUA KWA MATENDO YAKE SIO KWA KUAMBIWA MAAANA WOTE TUNAONA.
   
Loading...