Utalii wa uwindaji na hatma ya Tanzania

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Ndugu wana Jf
Leo ntachambua kidogo kuhusu utalii hapa kwetu Tanzania,ni ukweli kuwa utalii ni moja ya vyanzo nyeti vya mapato hapa nchini,lakini pia umechangia kukuza ajira kwa watanzania wengi,na huu ni utalii wa picha(photographic tourism)
hoja yangu ni jinsi serikali imeshindwa kuweka mikakati ya kuboresha sekta hii nyeti,kwa muda sasa serikali imeendelea kutoa vibali vya uwindaji pasipo kuwa na usimamizi wa kutosha wa wataalam wazalendo,ukweli ni kuwa wanyama wanaowindwa ni wale wale walioko hifadhini,maana hifadhi zipo wazi,kumekuwa na uwindaji mkubwa kuliko idadi sahii y a wanyama,hali inayopelekea kupoteza kabisa baadhi ya wanyama,eg idadi ya faru kwenye mbuga ya serengeti imepungua kutoka faru 10 per square km hadi faru 30 nchi nzima,hali hii si ya kukubalika,kwa wenzetu kama Kenya,africa kusini msumbiji etc wamekataa kabisa hii biashara,natoa wito kwa viongozi wetu kutunga sheria ya kuharamisha uwindaji ili kuokoa maisha ya wanyama
nawasilisha
 
Tatizo la msingi la utalii nchini ni viongozi wabovu na wasio hata na elimu ya utalii hali inayopelekea kuwepo na maamuzi mufilisi,,dawa yao ni peoples power
 
Back
Top Bottom