Utalii Wa Ajabu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utalii Wa Ajabu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Idimi, Nov 28, 2007.

 1. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #1
  Nov 28, 2007
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,217
  Likes Received: 2,078
  Trophy Points: 280
  Habari hii nimeinyaka jana, na nikawa naulizwa kama ni ya kweli. Sikuweza kukana wala kukubali, lakini ina ukweli fulani ndani yake, kwa sababu hii hata katika fukwe za Tanzania kama vile Zanzibar, Dar na Bwagamoyo ipo sana tu.
  Soma,


  OLDER WOMEN JOIN KENYA'S SEX TOURISTS
  Najua kutakuwa na mawazo mchanganyiko katika hoja hii, lakini hebu tuijadili kwa undani, kwani vijana hao wa Mombasa ni sawa kabisa na wale wa pale Bwaganoyo ama Zanzibar wanaowachukua wazungu wazee, kwa hiyo madhara ama faida ni zile zile.
  Vijana hawa waliotajwa hapo ni wadogo sana kiumri, yaani miaka chini ya thelathini, lakini vibibi wanavyochukua ni ajabu, miaka 56 na kuendelea. Pamoja na kwamba tunasema "Age Aint Nothing, but a Number" lakini tungalie madhara ya ngono hizi.
  Hoja zangu mimi ni kwamba, kwanza, huenda hawa wazee wana magonjwa kutoka kwao, kwa hiyo huyaleta kwa hawa vijana kwa kuwapa pesa kibao za kujikimu, hivyo vijana hawa husahau kabisa suala la kuambukizwa. Nijuavyo, kutokana na uzoefu, sio wazungu wengi wanaopenda matumizi ya mipira ya kiume, kwa hiyo huenda vijana hawa wakaiga mkumbo huo kwa kwenda 'dry' na kuangamia vibaya (kumbuka hiyo story hapo juu, kijana anasema kalamba kama wazungu 100 hivi).
  Pili, kuna hili suala la vijana kusaka "Makaratasi" ama viza, kwa maana ya pasi za kwenda majuu kwa kufanya mapenzi na hawa wazee, na baadaye kuwarubuni hawa wazee wawachukue na kwenda nao majuu kuwastarehesha, baadaye hawa vijana wanawatelekeza hawa wazee wakishafika huko, na kubakia wakiwa tayari wana makaratasi. Hii si haki. Hii nimeishuhudia, sihitaji kusimuliwa!
  Tatu, kijana wa kiswahili aishachukua mzungu, dada zetu nao humpapatikia kwa sababu wanajua atakuwa ana dola za kutosha, kwa hiyo mzunguko wa ngono unaendelea. Kama ni ugonjwa basi huyu dada wa kiswahili anakuwa ashaubeba.

  SWALI:
  Je huu ni utalii tunaoutaka hapa Afrika? Ni wa Kimaendeleo?
   
Loading...