Utalii tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utalii tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mjukuu2009, Nov 19, 2009.

 1. m

  mjukuu2009 Member

  #1
  Nov 19, 2009
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Habari wana JF,
  Kuna kitu kina nishangaza sana kuhusu serikali ya Tanzania,ata siku moja uwezi ukaona utalii wa Tanzania unatangazwa kwenye CNN au BBC sijui kwanini!?
  Lakini wenzetu kama Misiri wana vivutio vichache lakini wamevitangaa dunia nzima,akuna mtu asiyejua kuwa pyramid yanapatikana Misiri duniani.

  • Sisi wa Tanzania tuna mlima mkubwa africa (Kilimanjaro) watu duniani wanajua uko kenya tunapata shida kweli kuwa ambia watu nchi tuliyotoka mpaka utaje kenya ndio wanakuelewa,
  • Tuna mbuga za wanyama za kutosha kama vile Gombe,serengeti,selou na nyingine nyingi tu lakini azijulikani kimataifa,Animal movies karibia zote zilizoongoza kwa mauzo duniani zimerikodiwa kwenye mbuga zetu lakini akuna anae jua wala anayefuatilia ilo.
  • Tunamaziwa makubwa ya kihistoria kama ziwa tanganyika,victoria,nyumba ya mungu,ziwa nyasa na mengine mengi tu lakini amna mtu anaye jua duniani.

  • Tuna miji ya kihistoria kama kilwa,unguja,bagamoyo n.k akuna mtu anayejua duniani kama kuna sehemu nzuri za utalii Tanzania.
  Wana JF mlioko ndani na njee ya Tanzania naomba tusaidiane atakutangaza nchi yetu kimatifa kwani serikali iliyopo madarakani imesha shindwa ili zoezi kwa zaidi ya miaka 45.
  Asante;
   
Loading...