fakhbros
JF-Expert Member
- Sep 14, 2013
- 382
- 654
Kipaji ni tunu hakuna awezae kumzawadia mwingine kile alichopewa na manani
Fikra na ndoto zangu nilitegemea kuwa mcheza netball maarufu kama alivyo samata katika soka
Siku timu yetu ilipoweza kuifunga timu ya shule ya jirani hakika nilikuwa mfungaji miongoni mwa wafungaji wa magoli sitini mtaani na shuleni walimu walinipenda kwa aina yangu ya uchezaji
Kipaji changu hakikutambulika nyumbani sababu michezo ya aina hiyo haikuwa sehemu ya utashi wa wazazi, wao hawakujua michezo ya aina hiyo hasa kwa jinsia yangu
Mama alinifunza kucheza msita na dama na wakati mwingine tulikuwa tunaruka kamba na kuimba bayshow I love u
Mchezo wangu haukuwa maarufu pale kijijini kwetu kuliko ulivyokuwa maarufu mchezo wa soka
Zilikuwepo ligi za Jogoo ilitwa jogoo ligi
Ligi ya mbuzi na kondoo iliitwa meeee ligi ulipofika msimu wa uchaguzi ilianzishwa ligi ya diwani, mbunge, na hatimae ligi ya Rais ikiitwaa kazi kazi ligi
Washindi wa ligi ya kazi walizawadiwa vyeo kwenye KATA yetu na wengine walitunukiwa nishani iliyoitwa tuzo ya utepe wa kijani
Japo mchezo wetu pindi tulipokusanyika kwenye viwanja vya netball washabiki wetu walikuwa ni wazee na vijana wa pale kijijini shangwe na ndelemo zilitwala pale ambapo mtu angeruka juu na kichupi kuonekana basi ungesikia yowe kutoka pembezoni
Hakika japo niliupenda sana mchezo wa netball kwangu ulikuwa mchezo wa ndoto zangu nilitamani kuona club kubwa ya netball ikiitwa Simba netball club naamini kwa umahili wangu wa uchezaji ningeweza kusajiliwa pale kama Mavugo ambae uchezaji wake sidhani kama ananizidi Mimi naamin kama Simba netball club wangeweza kuja kijijini kwetu Itobo wangeniona na mkataba wangenipa haraka
Usiku wa usajiri kwenye kipaji changu haukuwa kama zilivyokuwa ndoto zangu
Kutokana na utamaduni wetu hadhi yakuolewa ilikuwa ni hadhi kubwa ndani ya jamii yetu,
Nilijikuta baada ya kuhitimu masomo yangu ya darasa la saba hapakuwepo nafasi yakuendelea kucheza mchezo nilioupenda
Kumbe tayari baba alikuwa amefatwa na wazee mbalimbali wa pale kijijini waliohitaji vijana wao wanioe kutokana na umahili wangu ktk uchezaji nadhani walifikiri kama ningeolewa na vijana wao basi kizazi chetu kingeweza kuwa kizazi cha kurukaruka kama nilivyokuwa mahili katika mchezo huo wa netball..
Nimeyaishi maisha ya netball hata baada ya ndoa ni miaka 52 ya ndoa yangu nikiendelea kuiota ndoto yangu naamini ipo siku nitasajiriwa nirudi uwanjani.