stwita
JF-Expert Member
- Feb 14, 2011
- 1,340
- 761
Leo kwenye lunch kazini kulikuwa na mjadala juu michepuko na njia kuu kwa wapenzi wapya ambao labda wako pamoja kama mwaka mmoja hivi inawezekana hata wanaishi mikoa tofauti. Hoja kadhaa za kufanya mtu ajitambue kama yeye ndio mchepuko au njia kuu zilitoka, naomba tuongezee zaidi hoja za hapo chini ili wengi tujifunze.
Kama unaona dalili zifutazo kwa mpenzi wako tambua kwamba inawezekana wewe ni mchepuko, tena usiyependwa na unapotezewa muda wako tu;
Mpenzi wako wa Kiume (wewe ni wa kike)
1. Hapendi umpigie simu na ukipiga hapokei hadi yeye atakapoamua kupiga na mkiongea ni dakika chache sana
2. Anachukua muda mrefu kujibu text zako hata kama umetuma kwa viber, whatsapp na ikawa delivered na anaonekana yuko online, hajibu mpaka atakapoamuana akijibu inakuwa fupi sana na iko dry mfano
Wewe:Hello love
Yeye: Kimya ,
siku 2 baadaye
Wewe: Mambo
Yeye: Kimya
Jioni siku hiyohiyo
Yeye: Hey there
Wewe: hey stranger, missing you
Yeye: Ha ha
END OF CHAT hadi wewe uanzishe tena mawasiliano,usipoazisha zinaweza hata pita wiki 2 kimya kimya
Chat kama hiyo inarudia mara kwa mara, inakuwa ndiyo routine yenu
3. Hapokei simu zote mbele yako, ataenda kando kabisa ili usisikie anachoongea, kama kuna mlango ataufunga
4. Kwenye simu yake hajai -save namba yako na kama amei-save hajai-save kwa jina lako unaweza kuwa umendikwa NGO,SACCO au Bank n.k
5. Haoneshi shauku ya kuwa na wewe mara kwa mara, hata zikipita wiki yeye hajali ila siku akiwa ana hamu ya sex na wewe atakutafuta popote pale, ashiki zake zikiisha anaondoka haraka.
6. Hajawahi kukuonesha kwake, siku akikuahidi kukupeleka anapata dharura dakika za mwisho
7. Hajawahi kukutambulisha kwa rafiki yake hata mmoja licha ya ndugu yake yoyote pamoja na kwamba mko wote kwa zaidi ya mwaka
8. Siku mkitoka, mnatoka usiku tu,hakuna lunch dates
9. Hapendi ujue mambo yake, hata akisafiri hakuagi
10. Hazungumzii mwelekeo wa mapenzi yenu, discussion yenu huwa ni CHADEMA, CCM, UKAWA, Katiba Mpya, Muungano,Serikali, dini, el shabab,matukio na mambo mengine kama hayo (japo sio mbaya kuwe na balance basi)
11. Mnaishi mikoa tofauti, kwa bahati wote mnasafiri kwenda Moshi kwa kuwa mawasiliano yenu ni nadra, ukifika Moshi unamfahamisha kwamba uko Moshi kikazi bila kujua kama na yeye yuko Moshi. Anaonesha kufurahi,mnapanga kukutana, hatokei, no warning,no apology, hapo mlikuwa hamjaonana miezi kadhaa
ONGEZA NYNGINE
Mpenzi Wa Kike (wewe wa kiume)
1. Hajibu text au hapokei simu, akiulizwa kachoka
2. Hana wivu kabisa na wewe
3.Hapendi kuongozana na wewe barabarani
4. Hana haraka ya kujua ndugu, marafiki zako kwa ufupi hana interest kabisa na maisha yako
5. Haoneshi hisia za mapenzi juu yako, anakuwa kama anajilazimisha kuwa na wewe
6. Anakutafuta anapohitaji msaada wako tu au pesa
7. Anakosoa kila kitu kuhusu wewe
8. Anaanzisha ugomvi mara kwa mara
9. Hakutumii text wala kukupigia simu
ONGEZA NYINGINE
Tuacheni hizi jamani, kama mtu humpendi bora kumwambia ukweli mapema kuliko kumpotezea muda wake na kuja muumiza baadaye,haya maisha mafupi.