Mwizi kamwona jamaa kabeba begi ndogo mkono,akamnyemelea taratibu na hakujua kwa jamaa kashikilia vizuri,ile anampokonya mvutano ukaanza,jamaa haachii na mwizi haachii,kila mtu anasema begi langu,mara polisi akatokea akawapeleka kituoni,akaanza kuwahoji,kila mmoja anasema begi langu,mwenye begi akamwambia polisi naomba niruhusu dk 30 nichukue risiti niliyopewa baada ya kununua begi,polisi akamruhusu jamaa.
wamesubiri weeeeee jamaa harudi,mwizi akaanza''si unaona jamaa harudi,nilishakuambia begi ni langu,nipe begi langu''
Polisi akaamua afungue begi ili aone kuna nini,alipofungua kidogo azimie mana kulikuwa na kichwa cha mtu.
mwizi akaanza ''nakuomba nakuomba mi siyo mwenye begi,mi ni mwizi,kazi yangu ni kuiba begi si langu,nisamehe mi si mhusika''