Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,611
Kiwango cha juu cha homoni, ambayo husababisha kuongezeka kwa kiwango cha magonjwa ya asubuhi katika kipindi cha wiki mbili za kwanza za ujauzito wakati mwingine unaweza kupata ugonjwa wa asubuhi kujulikana kama “hyperemesis gravidarum” na pia kichefuchefu.
Ujauzito wa mapacha unaleta uchovu sana, kulala, na kujisikia vibaya, wiki mbili au tatu za mwanzo za ujauzito. Kulisha watoto wawili inahitaji usingizi wa kutosha na chakula bora kwa ajili ya mwili wako ili uweze kufanya kazi vizuri.
Hamu ya kula inaongezeka, kwani mwili wako unahitaji chakula cha kutosha kwa ajili ya kukuza watoto vizuri
Mfuko wa uzazi huwa mkubwa kwasababu umebeba zaidi ya kiumbe kimoja,hii inasababisha tumbo kuwa kubwa.
Mabadiliko ya jinsi unavyojisikia ni kitu cha kawaida kwasababu kiwango cha homoni kinaongezeka ili kuweza kustaimili ukuaji na maendeleo ya watoto, hali hii inaonekana sana wiki sita tangu ujauzito.
Ujauzito hutambilika sana baada ya kipimo cha mkojo au damu,baada ya kipimo hichi unaweza kupata uhakika kama una ujauzito wa kawaida au wa mapacha. Vilevile ujauzito wa mapacha unapelekea kuwa na mstari tumboni wenye rangi iliyokolea.
Tukiachana na hizo kuna ishara nyingine ambazo zinatofautisha ujauzito wa kawaida na ule wa mapacha.
Ishara zaidi za ujauzito wa mapacha
Kulingana na ishara za mwanzounaweza kutambua kama una ujauzito wa mapacha .lakini kuna ishara zaidi zinazoweza kukupa muafaka zaidi:
Wakati una ujauzito wa mapacha unaweza kuongezeka uzito haraka sana kuliko kubeba mtoto mmoja tu. Uchunguzi wa mara kwa mara wa daktari wako unaweza kukusaidia kujua umri wa mtoto na ukuaji wake, kama kipimo hiko kinaongezeka kwa sentimita moja kila wiki basi ni ishara moja kuwa unatarajia kupata mapacha. Kusogea kwa mtoto tumboni hutokea mapema sana wakati ukiwa na ujauzito mapacha kuliko mtoto ule wa mmoja.
Kuelekea mwisho wa miezi mitatu ya kwanza, daktari anaweza kuchukua kipimo kiitwacho “Doppler heartbeat count” kuweza kutambua mapigo ya moyo ya mtoto. Kama umebeba mapacha utasikia mapigo ya moyo mara mbili.
Ujauzito wa mapacha huambatana sana na kukosa pumzi, hii ni kwasababu ya ukuaji wa mfuko wa uzazi unaobana mapafu hivyo kusababisha kukosa hewa.
Nyonga kuuma ni ishara mojawapo ya ujauzito wa mapacha kwani kukua kwa mfuko wa kizazi kusio kwa kawaida husababisha nyonga kuuma kwani uzito unaongezeka na kukandamiza nyonga.