Umekwenda church na ulipokaa pembeni yake amekaa mpenzi wako wa zamani uliyemfuma live na boya mwingne then mkaachana. Mhubiri anawambia waumini mtizame wa pembeni yako mwambie "NAKUPENDA"
Afu hiyo style ya kuwaambia waumini mgeukie jirani yako afu mwambie hivi ilishawahizua balaa. Ilikuwa hivi, dogo mmoja alikuwa kakaa na dingi yake karibu, mchungaji alikuwa anahubiri kuhusu wale wote ambao hawajapata kuzaa na akasema Mungu atatenda miujiza na watazaa, akasema mgeukie jirani yako mwambie "leo utapata mimba".Mara kikaskia kichapo cha maana, kumbe dogo alimgeukia dingi yake akamwambia "leo utapata mimba"