Utajiri wa Lowassa unavyoyatesa makanisa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajiri wa Lowassa unavyoyatesa makanisa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, May 20, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  May 20, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  KATIKA mafundisho ya Injili, ambayo ni maelezo kuhusu Yesu Kristo, inaelezwa kwamba mama mmoja alikamatwa na kupelekwa mbele ya Kristo akituhumiwa kufanya ukahaba huku wadau waliomkamata wakimtaka Kristo kutoa hukumu ili mama huyo aadhibiwe kulingana na maelekezo ya torati.
  Kristo alitumia hekima yake na kusema sawa, anayejielewa ni msafi hajapata kutenda kosa la jinsi hiyo na awe wa kwanza kutoa adhabu husika. Kauli hiyo iliwafanya watu wote kutawanyika huku Kristo akimwambia mama yule aende zake na asirudie makosa yale.
  Tunaona kwamba Kristo hakutumia njia yoyote kujinufaisha na udhaifu wa mwanamke huyo zaidi ya kutoa fundisho kwamba tunapohukumu ni lazima kwanza tujitazame sisi tuna usafi gani unaotuhalalisha kuwahukumu wengine.
  Hapa nchini kwetu kuna aina ya kashfa ambayo imetokea kufanana na makosa yanayotajwa kwenye torati kama makosa ya mauti, ufisadi. Kama ilivyosemwa kwenye torati kwamba mzinzi anapaswa apigwe mawe mpaka afe, hata ufisadi unaonekana kuchukiwa kiasi cha kufananishwa na uzinzi kwenye torati, fisadi anatazamwa kwa jicho baya sana na Watanzania kwa sasa.
  Wapo watu wanafanya ufisadi na kujinufaisha nao lakini huku wakiunyanyapaa, hawataki kujiita wala kujulikana kwamba ni mafisadi.
  La kushangaza ni kwamba ufisadi unaonekana ni mbaya, mchafu, watu hawautaki wala kuhusishwa nao, lakini hawakomi kuufanya! Kwa kuufanya ufisadi ni mtamu ila anayeufanya anaona aibu kuitwa fisadi!
  Mtu anayeitwa fisadi, hata kama anajielewa kuwa anaufanya ufisadi, tena kwa makusudi, na akielewa kwamba ananufaika nao, atapiga kelele kwamba anatukanwa, anaonewa wivu na mambo mengine ya kuipinga sifa hiyo ambayo kila mmoja wetu anaiona ni mbaya isiyofaa kwa mtu kutambulishwa nayo katika jamii.
  Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa (CCM) jamii imemuweka wazi kuwa ni fisadi. Sitaki kumhukumu kwa vile sina ushahidi wa kutosha wa kunifanya nimuone hivyo. Ila nitasema kile ambacho jamii inakichukulia kama ukweli kumhusu.
  Lowassa ni mtumishi wa muda mrefu katika serikali na baadaye akawa Waziri Mkuu kabla ya kujiuzulu kwa kashfa ya kuipa zabuni ya ushindi kampuni ya kuzalisha umeme wa dhararua ya Richmond.
  Wapo wanaomuandama Lowassa wakitaka asulubiwe kwa kashfa hiyo ya ufisadi sawa na mwanamke aliyepelekwa kwa Kristo akituhumiwa kwa ukahaba. Lakini hata hivyo wanaobeba tuhuma hizo dhidi ya Lowassa hakuna hata mmoja anayeweza kututhibitishia kwamba ni msafi asiyepata kutenda kosa kama lile analotuhumiwa nalo Lowassa.
  Kwa hapo fundisho la Kristo ndipo linapochukua nafasi yake kwamba asiyepata kufanya au kuhusishwa na ufisadi na awe wa kwanza kumsulubu Lowassa.
  Ninalotaka kuliangalia katika makala haya ni namna Lowassa alivyoingia katika mbeleko ya kanisa na kanisa kumuwekea kinga, lakini kinga iliyo tofauti na ya Kristo kwa mwanamke aliyedaiwa ni kahaba.
  Kristo aliposema kwamba anayejijua ni msafi na awe wa kwanza kurusha jiwe kutekeleza sheria ya torati ya kumpiga mawe mzinzi mpaka afe, alijikuta amebaki na yule mwanamke peke yake baada ya watu wote kutawanyika kwa aibu.
  Kumbe watu wote walikuwa wakilitenda kosa lile. Baada ya hapo ndipo Kristo akamuasa mwanamke yule kutorudia makosa yake. Yule mwanamke akawa ameshinda kesi kwa njia ya aina yake.
  Lakini linapokuja suala la kanisa na Lowassa tunaona kitu kilicho tofauti kabisa. Kanisa linapinga ufisadi, ila linajaribu kutumia mbinu kama aliyoitumia Kristo kumnusuru mama mzinzi. Pamoja na ukweli huo kanisa linashindwa kumwambia Lowassa nenda usirudie kutenda makosa haya.
  Baada ya kutaka kumnusuru Lowassa kwa njia ya Kristo kwa mwanamke mzinzi Kanisa linang'ang'ani kubaki na Lowassa kwa manufaa yanayoonekana ni ya Kikanisa. Kanisa linaonekana kumweka Lowassa kwenye mbeleko yake na kuzunguka naye kila pahala, kitu kinachoonekana kama vile kanisa lina namna linavyojinufaisha na tuhuma zinazomkabili mtu huyo.
  Katika nyakati tofauti tumeshuhudia kanisa likimualika Lowassa katika shughuli zake mbalimbali kana kwamba bila yeye kufika shughuli hizo haziwezi kupata baraka za Mungu!
  Ndiyo, tumeishapata somo kwamba kutuhumiana si kuzuri. Kristo alisema kwamba anayejua kwamba hajatenda kosa kama lile na awe wa kwanza kutoa adhabu husika. Lakini hata hivyo Kristo hakufundisha kwamba tunaweza kujinufaisha na tuhuma zinazomkabili mtu.
  Kwahiyo kama kanisa linamuona Lowassa hana hatia basi lingemwambia nenda zako usirudie kufanya au kujihusisha na kashfa za aina hiyo na kisha kuachana naye.
  Lakini kitendo cha kanisa kuandamana na Lowassa karibu kila pahala likijinufaisha na michango na misaada anayolitolea kinatoa picha kwamba Lowassa anatiwa nguvu na kanisa ili aendelee kupata kwa njia anayotuhumiwa nayo huku akiwa amelindwa na kanisa. Kwa maana nyingine kanisa linamtia Lowassa ujasiri mpya ili kama ni ufisadi aendelee kuufanya kwa nguvu na kasi mpya!
  Hakuna namna ambayo kanisa linaweza kusema kwamba linaupinga ufisadi ilhali likimtegemea mtuhumiwa wa ufisadi aliwezeshe kwa namna mbalimbali kwa kukitumia kile anachotuhumiwa nacho.
  Utasikia Lowassa kaalikwa katika kutunisha mfuko wa kanisa fulani, mara kaalikwa kwenye uzinduzi wa ujenzi wa kanisa, mara ujenzi wa kigango, kutiwa wakfu, uzinduzi wa kwaya nakadhalika. Na kote huko mwalikwa huyo anamwaga mapesa au ahadi.
  Kwa nini kanisa halijiulizi mtu ambaye kwa muda wote wa maisha yake amekuwa mtumishi wa serikali fedha zote hizo anazipata wapi? Kwa nini hiyo isiwe njia ya kulifunua kanisa macho na kuanza kukiona kile ambacho mtu huyo anatuhumiwa nacho?
  Kwa njia hiyo tunawezaje kukosa kuamini kwamba katika fungamano la makanisa na Lowassa kuna kitu ambacho kimejificha ndani yake, kitu ambacho kinawezekana kuwa ni mpango wa nilinde nikulinde? Kwa nini mtu ambaye anaandamwa na tuhuma za utajiri mchafu aonekane msafi kwa kanisa na kubebwa kila mahali akiwa amepewa kipaumbele?
  Kama nilivyoonyesha mwanzo kuhukumiana kwa tuhuma tu ambazo hazikuthibitishwa si jambo jema, hata Kristo alionyesha kutokubaliana nalo. Lakini vilevile kujinufaisha kwa kumkingia kifua mtuhumiwa nalo si jambo jema, sababu tunaona kwamba hata Kristo hakufanya hivyo.
  Kwahiyo ingefaa kanisa litoe maelezo ya kwa nini lisihusishwe na ufisadi baada ya kuonekana linambeba mtu anayetuhumiwa kwa ufisadi na kumkingia kifua huku likiwa linajinufaisha naye kwa njia mbalimbali.
  Pamoja na hilo mtindo wa kanisa kutaka waamini wake watoe asilimia kubwa ya vipato vyao kwa kanisa bila kujali vyanzo vya vipato hivyo ni dosari kubwa kwa kanisa. Kuna uwezekano mkubwa kanisa likajikuta linauchochea ufisadi, hata ujambazi, kwa kuvibariki vitu vilivyopatikana kwa njia hizo haramu baada ya vitu hivyo kutolewa kanisani kama sadaka takatifu.
  Mtazamo wangu ni kwamba kanisa lingetakiwa kujitenga na tamaa inayoweza kulifanya lionekane linashadidia uasi kwa kuwakumbatia tu watu wenye mali kana kwamba inatangazwa kwenye Injili kwamba wenye nacho ndio watakaoupata ufalme wa mbinguni.
  Injili inatueleza wazi kuwa tajiri kufika mbinguni ni vigumu kuliko ngamia kupita kwenye tundu la sindano. Kwa kulizingatia hilo inabidi tujiulize kanisa linapata wapi ujasiri wa kuwakumbatia matajiri, ambao tayari wanaonyeshwa kwamba kuupata ufalme wa mbinguni ni kitu kigumu kwao, badala ya kuwashauri wakagawe mali zao zote kwa masikini na kumfuata Kristo kama Kristo mwenyewe alivyomshauri Zakayo? Ikumbukwe Kristo hakumwambia Zakayo kwamba utajiri wako wote leta kwamgu. Alimshauri akaugawe kwa masikini.
  Kwa mtazamo huo ningeweza kulielewa kanisa kama lingempa Lowassa ushauri wa kuachana na utajiri wake kwa kuwanufaisha maskini ili yeye apate kuokoka kuliko kanisa lenyewe kujinufaisha na utajiri huo wa Lowassa ambao ni kama unalinajisi hekalu hilo la Mungu.
   
 2. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2013
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Lowassa anapiga kote kote nguvu ya fedha ni nguvu ya giza hupendwa na na wengi kwani hakuna kuabudu Mungu tena bali vito, thamani na fedha
   
 3. k

  kilombero yetu JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2013
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,007
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  rafiki yetu karugendo,kama una ushahidi wa ufisadi wake wewe tuletee ili tumshughulikie
   
 4. m

  mkweli44 New Member

  #4
  Jul 8, 2013
  Joined: May 7, 2013
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  prudencekarugendo@yahoo.com 0784 989 512

  Ndugu prudence;uchambuzi wako hauko realistic pia napata wasiwasi na uelewa wako. Watu kumtuhumu mtu si kigezo cha kuwa mtu huyo tayari ni mkosaji na hasa ukizingatia mazingira ya kisiasa nchi Tanzania. Kwani wewe hujawahi kushutumiwa na watu maishani mwako?je ni kweli kuwa yote ambayo watu waliokaribu na wewe wanasema juu yako ni ya kweli? unasema hata wewe ukiambiwa uthibitishe ufisadi wa lowassa huwezi, iweje uyatake makanisa yamchukulie yeye kama fisadi?. Tuthibitishie ufisadi wa lowassa,toa takwimu za utajiri wake unaodai anawao kiasi cha kuitikisa nchi. au wivu ndo unakusumbua?. Nani kakuambia kuwa pesa zote katika harambee anatoa yeye?.kuhamasisha watu wachangie maendeleo ni kosa?. Nakushauri ndugu yangu kuwa na mawazo huru. zingatia hoja zaidi kuliko mihemko ya watu.
  Mimi binafsi namkubili lowassa kwa kila anachoongea ni realistic.nani hajui kuwa elimu ni tatizo Tanzania?.matatizo yanayowakabili machinga yapo wazi. Ishitoshe katika nchi inayozinagatia utawala wa sheria,mahakama ndo chombo kilicho eligible kumtia mtu hatiani. Hayo yote juu ya lowassa ni wazi ni chuki,wivu na kutapatapa. The guy is charismatic and seem to be serious na ana uchungu na matatizo ya watu.
  Ushauri kwa Lowassa
  Mheshiwa (lowassa) usivunjwe moyo wa watu wenye mawazo finyu.Endelea kuhimiza watu katika maendeleo. Watapigana lakini hawatakushinda.Ushawishi wako na kukubalika kwako ni wazi kuwa Mungu yupo upande wako. Pia watu wote makini wapo na wewe. Stay blessed.

   
 5. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,026
  Likes Received: 1,396
  Trophy Points: 280
  Hatareeeeee
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2013
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,818
  Likes Received: 83,217
  Trophy Points: 280
 7. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2013
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,659
  Likes Received: 4,755
  Trophy Points: 280
  Laigwanani noma kaingia hadi misikitini kuomba kura.
   
 8. G

  GERVAS MILEHE Member

  #8
  Jul 8, 2013
  Joined: Jun 16, 2013
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  unaweza kutuambia sababu 1,2,3 za lowwasa kujiuzulu?
  km alikuwa hana tuhuma,ni waz anawajua mafisad wenzake,mbona hakuwataja?
  ww hata umpende vip,watz wote wanajua lowasa FSD,hafai kuongoza hata nyumba 10!
   
 9. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #9
  Jul 8, 2013
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Makanisani nako siku hizi wapenda pesa wengi mno, kifupi ni kama watumishi hao wa mungu nao ni wezi tu. UCHU A PESA HATA MAKANISANI? aibu aibu, pesa ilimua yesu sasa makasisi nao ukiwa na pesa hata kama una wake 7, mwizi mkuu kama EL tapeli kama RA bado ukitoa mchango wa kitita utapewa nafasi ya mbele AIBU KWA MAKANISA AICT, RC, KKKT, MOROVIAN, ANGLIKAN etc
   
 10. z

  zamlock JF-Expert Member

  #10
  Jul 8, 2013
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  siyo makanisani tu mpaka misikitini pesa haramu zimeingizwa kazi kweli kweli yetu macho watanzania wanao sahau mara kwa mara
   
 11. Elungata

  Elungata JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2013
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 28,052
  Likes Received: 8,540
  Trophy Points: 280
  Hivi lowasa alifanyaga ufisadi gani ?maana kila siku wanasema visadi lakini hawasemi alifisadi wapi na shs ngapi.
   
 12. TECHMAN

  TECHMAN JF-Expert Member

  #12
  Jul 8, 2013
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 2,677
  Likes Received: 162
  Trophy Points: 160
  Siku tisini za Nape zinaisha lini jamani? Au tulikosea kumsoma alisema miaka tisini?
   
 13. p

  pembe JF-Expert Member

  #13
  Jul 8, 2013
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 2,058
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mbona watushangaza? huyo Mh anaweza kuwa fisadi au sio fisadi sisi watu wa kawaida hatujui utajiri alio nao Lowassa, labda atuambie yeye kama hana akaunti huko Uswisi. La msingi ni kuwa alikuwa waziri mkuu na akashindwa kuwajibika! Ndio sababu akaachia ngazi. Lile la kuwafukuza wazung wa DAWASCO alifaulu lakini la Richmond likamshinda. Sasa kujipitisha pitisha makanisani na misikitini linatutatiza kwani yeye kama mwanasiasa anachotafuta huko ni nini? Apande kwenye majukwaa atuambie wananchi la Richmond lilinishinda lakini mkinipa kura nitakuwa Raisi wenu mchapa kazi na sitarudia maksosa kama yale ya Richmond.
  Talanta aliyo nayo ni kama ya Mh Lyatonga Mrema!
   
 14. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #14
  Jul 8, 2013
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  Hivi ni RICHMOND ipi ?,ile ya pale UBUNGO juzi iliyotembelewa na MUME mkubwa, au ya UPANGA mtaa wa Mindu?
   
 15. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #15
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  kwanini uwaziri mkuu ulimshinda akaamua kujitoa bila kufukuzwa?
   
 16. K

  KIM KARDASH JF-Expert Member

  #16
  Jul 8, 2013
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 5,083
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Richmond ile kampuni feki iliyopendelewa na lowassa na kupewa tenda lakini ikashindwa kudeliver kutokana na kutokua na uwezo!
   
 17. u

  uwemba1 JF-Expert Member

  #17
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 755
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 60
  Kavishwa joho maalumu na BAKWATA au hujasikia?? Tafuta uzi upo humuhumu. Aibu kwa BAKWATA
   
 18. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #18
  Jul 8, 2013
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  jamni hivi nani anaweza tuweka hapa jumla ya mihela tangua aloameanza kutoa hadi sasa.....tuanza kutafiri kazitoa wapi?
   
 19. isambe

  isambe JF-Expert Member

  #19
  Jul 8, 2013
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 2,053
  Likes Received: 881
  Trophy Points: 280
  ooooOOOH!!thanx kwa kunijuza,kwa hiyo walivyoshindwa kudeliver ilibidi na ile mitambo yao waiondoe pale Ubungo ndio ikaletwa hii ya sasa ambayo alikuja Aunt Hilary,na juzi Auncle Baraka katoka kuhisabahi???.
   
 20. CURRENT ISSUE

  CURRENT ISSUE JF-Expert Member

  #20
  Jul 8, 2013
  Joined: Jun 20, 2013
  Messages: 257
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  .

  Itabidi hili tuliongeze kwenye masomo ya theolojia au Mzee umepitia kidogo hayo?Usihukumu.
   
Loading...