Utajili maradufu huu hapa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utajili maradufu huu hapa.

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Mbaga Michael, May 10, 2012.

 1. Mbaga Michael

  Mbaga Michael Verified User

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 2,911
  Likes Received: 202
  Trophy Points: 160
  Habari wanajamii!

  Nawatafuta watu wenye mitaji ya kuanzia kama milioni 3 hivi tufanye nao biashara.

  Biashara yenyewe iko namna hii ni kuzalisha umeme kwa kutumia machine ya kusaga itakayobadilishwa na kuwa ya kufua umeme kwa kufungiwa moter, nipo eneo moja Mkoani mwanza pembezoni mwa mji ni sehemu iliyo na watu wengi sana kutoka sehemu mbalimbali za nchi wakiwa wamekuja kutafuta eneo hili, kwa bahati mbaya eneo hili hakuna umeme usambazwao na shirika letu la umeme la Tanesco bado haujafika, ingawa kuna mtu mmoja yupo sehemu hii ikijaribu kutoa huduma hii maeneo haya kwa kutumia machine ya kusaga yenye piston moja ambayo imeelemewa mzigo kwa mahitaji ya wateja kuwa makubwa hivyo kufanya watu kuendelea kukaa gizani


  hizi ndizo gharama anazozitoza huyu bwana kwa wateja wake kwa siku

  1. Ukihitaji umeme nyumbani kwako balbu moja tsh. 500/=@siku

  2. Kwa mwenye salon maeneo haya kama anahitaji hudumu yake anatozwa 3000/=@siku

  3. Kwa wenye kumbi labda za kuonyesha video tsh.5000/=@siku

  3. Kwa wenye maduka tsh.5000/=@siku kama ana charge na simu

  4. Kwa wenye mabaa tsh. 4000/=@siku huruhusiwa kutumia friji kuepusha mashine kuzimika kwa ukubwa wa mzigo

  kwa kifupi mahitaji bado ni mengi mno na hudumu iliyopo sasa inalegalega sana kama utalizika na maono yangu ya kufanya nawe mfanyabiasha biashara hii katika eneo ili tafadhari tuwasiliane kwa kuniPM
   
Loading...