Utaifa na uzalendo kwanza

MSHERWAMPAMBA

JF-Expert Member
May 22, 2014
341
119
Vyama vya kisiasa,ukabila,udini na ukanda visiwe ndio chanzo cha kututofautisha watanzania mpaka kufikia kukana maslahi au mambo yanayowahusu viongozi wetu wa nchi yetu.

Hivi siku hizi za karibuni baada ya mambo ya vyama vya upinzani kuwekwa wazi,umekuwepo upinzani dhidi na chuki kubwa dhidi ya nchi yetu na viongozi wake.

Kuna mifano mingi sana nimeiona hapa kijiweni inayoonyesha vijitabia ka hivyo.Mfano huu uliotokea juzi juzi wa sakata la Kagame na Rais wetu Kikwete,nimesoma baadhi ya watanzania hapa kijiweni kwetu,kujiengua na nchi yetu na kujiweka upande wa Kagame ,yaani watu kuonyesha sympath na wanywaranda zaidi ya nchi yetu.

Sisemi kuwa hakuna wenye uzalendo na uchungu wa nchi yetu humu,la kuna baadhi ya wabongo humu ndani mara nyingi uzalendo na uchungu wa nchi huviweka mbele zaidi ya vyama vyenu vya upinzani,yaani wakati mwingine nasoma baadhi ya threads na kushangaa kabisa kwa jinsi watanzania walivyogeuzwa na masuala ya udini na ukabila na vyama vyenu vya upinzani.

Watu wanamsifia criminal dhidi ya rais wetu wakati mwengine huwa nafikiria hapa kijiweni tumeingiliwa na mamluki wanaotaka kutuchafua na kutuharibia muelekeo wetu watanzania.

Nenda kwa wenzetu Kenya ukabila na udini ndi vinawala na wamechanganyikiwa kabisa,haya nenda Uganda story ni hiyo hiyo tuu,nenda Burundi nao wanahangaishwa na ugonjwa wa ukabila,nenda Rwanda huko ndio hakusemeki kwa chuki na mauaji ya watu bila sababu yaani hawa watu wanaingia nchi za watu kwa dhamira ya kwenda ua watu na kunyang'anya mali za watu mfano tunao na unajulikana na evidence zote ziko U.N na walifikia kutengeneza criminal organization na hilo group la majangili hao kuliita M23.

Haya si mimi ninayejaribu kuyazua inajulikana wazi wazi ni black and white na nani anajulikana yuko nyuma ya hili kundi na tunajua direction zote zinatoka kwa nani (anajifahamu)Sasa kumalizia sisemi kama sisi watanzania ni watu wasafi sana nasi tunamatatizo yetu lakini huwezi ukalinganisha na most of those countries mentioned above.

Uzalendo tuuweke wazi tusigawinyike wakati manufaa ya nhi yetu yamo matatani,kuna wachangiaji kama vile Jokakuu na Mkandara hawa jamaa pamoja na wengine kama wao wanaonyesha uzalendo wa hali ya juu wakati wa kujadili mambo yanayohusu maslahi ya nchi yetu kipenzi,nimewafuatiliya sana katika baadhi ya topics humu ndani.

Chuki zimekuwa ni kubwa sana dhidi ya wabongo,hii ni kwasababu makwao mambo sio kama kwetu,huu ni wivu mtupu,stability yetu inawachanganya sana.Uzalendo na utaifa wetu tuuweke mbele ya kila kitu kwanza.M/Mpamba.
 
Vyama vya kisiasa,ukabila,udini na ukanda visiwe ndio chanzo cha kututofautisha watanzania mpaka kufikia kukana maslahi au mambo yanayowahusu viongozi wetu wa nchi yetu.Hivi siku hizi za karibuni baada ya mambo ya vyama vya upinzani kuwekwa wazi,umekuwepo upinzani dhidi na chuki kubwa dhidi ya nchi yetu na viongozi wake.
Unamaana CCM haina ukanda, ukabila na udini? Jibu swali hili nifunguke!

Hivi LUKUVI aliyeenda kanisani DODOMA na kusema tukikubali serikali tatu, Zanzibar itakuwa ni jamhuri ya KIISLAMU alikuwa amehama chama?
 
Bila utaifakwanza nchi itaparanganyika. Hawa wapinzani hasa ch.....ni wa kufutwa kwenye uso wa dunia
 
Unamaana CCM haina ukanda, ukabila na udini? Jibu swali hili nifunguke!

Hivi LUKUVI aliyeenda kanisani DODOMA na kusema tukikubali serikali tatu, Zanzibar itakuwa ni jamhuri ya KIISLAMU alikuwa amehama chama?
mkuu hapo kwenye red mbona wengine hatukusikia au ndo unajitoa ufahamu?...jitambue acha kisabengo.
 
mkuu hapo kwenye red mbona wengine hatukusikia au ndo unajitoa ufahamu?...jitambue acha kisabengo.

WAZIWAZI
Wewe acha unafiki.. Kama husikilizi vyombo vya habari, husomi magazeti, JF unaingia kwa ID mpya kila leo; TV huangalii huwezi kujua.
LUKUVI alienda kanisani DODOMA na kusema
tukikubali serikali tatu, Zanzibar itakuwa ni jamhuri ya KIISLAMU alikuwa amehama chama?
 
Back
Top Bottom