DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 12,622
- 28,459
Tafiti hii imebaini kuwa kuna matumizi mabaya ya dawa za kupunguza makali ya VVU (ARVs) ambazo kimsingi zimekusudiwa kwa matumizi ya binadamu pekee, sasa zimekuwa zikitumika kulishia wanyama kama kuku, nguruwe na ng’ombe katika baadhi ya maeneo ya Tanzania. Tabia hii siyo tu kuwa ni kinyume na maadili ya kisayansi, bali pia inaleta hofu ya kuibuka kwa usugu wa dawa (drug resistance) kutokana na mabaki ya dawa kwenye nyama, maziwa na mayai hali inayotishia afya ya binadamu.
"There is concern about ARV residues in animal products like meat, milk, and eggs, posing risks to human health."
Inaandika Tafiti Hiyo, Tafifi Hiyo ambayo Imefanywa na Dkt Zuhura I. Kimera, Dkt Peter Shimo, Dkt Emmanuel C. Balandya ,Dkt Mecky I. N. Matee and Lisa V. Adams.
Utafiti ulifanyika kwa njia ya uchunguzi na Kwenda Field Moja kwa moja (survey) kwa kutumia mbinu mseto (Mixed Programs).
Mahojiano ya moja kwa moja (interviews) na wafugaji, wauzaji wa dawa na wataalamu wa mifugo. Uchunguzi wa nyaraka na sampuli za bidhaa za mifugo sokoni. Uchambuzi wa maabara kubaini uwepo wa mabaki ya ARV kwenye nyama na maziwa.
Utafiti ulifanyika katika mikoa mitatu: Dar es Salaam, Iringa na Mbeya kwa sababu zilionyesha viashiria vya matumizi hayo kupitia ripoti za awali...
Takwimu zilionesha zaidi ya 35% ya wafugaji walikiri kutumia dawa kama Lamivudine, Efavirenz na Tenofovir au Mchanganyiko Wa TLE na TLD kwa ajili ya kuku na ng’ombe wao, wakiamini kuwa zinawaimarisha wanyama au kusaidia kupambana na magonjwa.
60% ya wauzaji wa dawa za mifugo hawakuwa na mafunzo maalum kuhusu tofauti kati ya dawa za binadamu na za wanyama.
Sampuli 25 za nyama na maziwa zilionyesha uwepo wa mabaki ya ARVs kwenye vipimo vya maabara.
Mikoa iliyoongoza kwa tatizo hili ilikuwa Mbeya (40%), ikifuatiwa na Iringa (33%) na Dar es Salaam (27%).
Utafiti huu umegundua kuwa:
Ninashauri
NAWASILISHA..
HUU ndo Utafiti wenyewe..

- Kuna matumizi ya ARV za binadamu kwa wanyama, ambayo hayajathibitishwa kitaalamu wala kisera.
- Matumizi haya yanafanyika kwa kificho, lakini yanaenea kwa kasi kutokana na imani potofu na uhaba wa dawa za mifugo.
- Kuna uwezekano mkubwa wa kuibuka kwa VVU sugu (resistant strains) iwapo matumizi haya yataendelea.
- Uwepo wa mabaki ya dawa kwenye bidhaa za wanyama ni tishio kubwa kwa afya ya umma.
Ninashauri
- Elimu kwa jamii na wafugaji kuhusu hatari za matumizi ya ARV kwa wanyama.
- Serikali iandae miongozo madhubuti na sheria kali kuhusu matumizi ya dawa, Za ARV ikiwa ni Pamoja na Ufatiliaji wa Kina juu ya Matumizi yake na kufanya Ufatiliaji wa Kina ya WaVIU wanaotumia Dawa hizo..Ikiwemo Pills Count kwenye Centre zote Nchini (CTC)
- Usambazaji wa dawa sahihi kwa mifugo kwa bei nafuu uwekwe kipaumbele.
- Ukaguzi wa mara kwa mara kwenye masoko ya bidhaa za wanyama kuhakikisha hakuna mabaki ya dawa hizi.
- Utafiti wa mara kwa mara kuendelea kufuatilia mwenendo huu na athari zake kiafya na kimazingira.
NAWASILISHA..
HUU ndo Utafiti wenyewe..