Sauti za Wananchi
Senior Member
- Sep 2, 2014
- 113
- 138
MUHTASARI
Ni siku 500 zimepita tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kuteua timu ya watendaji wakuu katika sekta mbalimbali. Kipindi hiki kinatosha kuwapa wananchi mwenendo wa vitendo vya serikali na kuona jinsi ambavyo aina ya uongozi huu unavyoyagusa maisha yaoya kila siku
Muhtasari huu umebeba maoni ya wananchi juu ya masuala ya kisiasa. Kwa mtazamo wao, ni tatizo gani kuu linaloikabili nchi kwa sasa? Je, tatizo hilo limebadilika ukilinganisha na miaka iliyopita? Je, wananchi wanauonaje utendaji wa viongozi wao, akiwemo Rais? Na je, kuna mabadiliko yoyote katika kukubalika kwa vyama mbalimbali vya siasa katika kipindi cha miaka michache iliyopita?
Takwimu hizi zilikusanywa kati ya tarehe 31 Machi na tarehe 17 Aprili mwaka 2017.
Matokeo muhimu ni:
• Wananchi wametaja umasikini/hali ngumu ya kiuchumi kama tatizo kuu linaloikabili Tanzania kwa sasa.
• Idadi ya wananchi wanaotaja upungufu wa chakula kama tatizo kubwa imeongezeka.
• Idadi ya wananchi wanaotaja rushwa kuwa tatizo kubwa imepungua.
• Tofauti na miaka iliyopita, ni wananchi wachache wanaokubali utendaji wa viongozi waliowachagua mwaka 2017.
• Asilimia 71 wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli.
• Asilimia 84 ya wananchi wanasema huenda watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.
• Asilimia 63 wapo karibu zaidi na CCM kuliko vyama vingine.
• Idadi ya wananchi wanaofungamana na Chadema imeshuka tangu mwaka 2013.
Fuatilia mubashara > LIVE - Yanayojiri Makumbusho ya Taifa: Utafiti wa Twaweza kuhusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini