Utafiti wa TWAWEZA: Rushwa imepungua lakini hali ya maisha imezidi kuwa ngumu

Sauti za Wananchi

Senior Member
Sep 2, 2014
113
138
MUHTASARI

Ni siku 500 zimepita tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kuteua timu ya watendaji wakuu katika sekta mbalimbali. Kipindi hiki kinatosha kuwapa wananchi mwenendo wa vitendo vya serikali na kuona jinsi ambavyo aina ya uongozi huu unavyoyagusa maisha yaoya kila siku

Muhtasari huu umebeba maoni ya wananchi juu ya masuala ya kisiasa. Kwa mtazamo wao, ni tatizo gani kuu linaloikabili nchi kwa sasa? Je, tatizo hilo limebadilika ukilinganisha na miaka iliyopita? Je, wananchi wanauonaje utendaji wa viongozi wao, akiwemo Rais? Na je, kuna mabadiliko yoyote katika kukubalika kwa vyama mbalimbali vya siasa katika kipindi cha miaka michache iliyopita?

Takwimu hizi zilikusanywa kati ya tarehe 31 Machi na tarehe 17 Aprili mwaka 2017.

Matokeo muhimu ni:

• Wananchi wametaja umasikini/hali ngumu ya kiuchumi kama tatizo kuu linaloikabili Tanzania kwa sasa.
• Idadi ya wananchi wanaotaja upungufu wa chakula kama tatizo kubwa imeongezeka.
• Idadi ya wananchi wanaotaja rushwa kuwa tatizo kubwa imepungua.
t1.PNG

• Tofauti na miaka iliyopita, ni wananchi wachache wanaokubali utendaji wa viongozi waliowachagua mwaka 2017.

t2.PNG

• Asilimia 71 wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli.

t3.PNG

t5.PNG

• Asilimia 84 ya wananchi wanasema huenda watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

t4.PNG

• Asilimia 63 wapo karibu zaidi na CCM kuliko vyama vingine.

t6.PNG

• Idadi ya wananchi wanaofungamana na Chadema imeshuka tangu mwaka 2013.

T8.PNG

Fuatilia mubashara > LIVE - Yanayojiri Makumbusho ya Taifa: Utafiti wa Twaweza kuhusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini
 
Attachments

  • SzW-TZ-Governance-June2017-EN-FINAL.pdf
    1.1 MB · Views: 78
Hivi hawa twaweza hizi tafiti wanafika kila kona ya nchi na vinijini au wanaishia mjini tu afu wanakuja na ripoti zao!
Mbona mie sijawahi kuwaona
 
Nimemsikia pole pole DW nae ametoa zake!
Anasema anakubalika kwa 83%
Nikagundua kumbe asilimia zikipungua wanatumia eeeh; kwenye zile 96 alipowapongeza twaweza mpaka mate yakakauka
 
kiasi kikubwa rushwa imepungua sana katika maofisi ya serikali na watu wamekuwa wakichapa kazi sana , imekuwa tofauti sana na miaka miwili nyuma , watu wamekuwa wanaheshim kazi , c toa kitu tufanye kazi , hilo natoa pongezi kwa serikali hii.
 
Mbona maajabu haya yani CHADEMA ikashuka kukubalika toka 32%-17% kuanzia mwaka 2013.Lakini cha ajabu mwaka 2015 wakapata 34% ya kura huku wale wenye 96% kura zikipungua toka 61% za JK mpaka 56% za baba Jesca.
Duh... Huu utafiti kibokoooooo
 
Kama ni hivyo ni sawa ila kwa nini maisha yazidi kuwa magumu??Au rushwa ilikuwa inarahisisha maisha???
 
Cha aabu kura zikaongezeka 2015, na wale maccm waliongezeka kwenye takwimu kura zikapungua.
duh!
kweli JAZA UJAZWE.
Magufuli alijipatia kura za wanaccm na ziada kidogo...unakumbuka wanaccm walikuwa wangapi?

Muone Zitto kwa maelekezo ya kuvuka mto Mara.
 
Hivi hizi Taasisi za Tafiti za uongo haziwezi kufungiwa kama Magazeti? Hizi ni Tafiti za Uongo. Labda waniambie tafiti zao hawajafanya Airport na Polisi.

Rushwa bado ipo sana na wala haijapungua maeneo niliyoyataja. Kama unanibishia, safiri pitia Airport ya Dar halafu zidisha mizigo uone. Au ukiingia Airport ya Dar halafu uwe na Mizigo mingi, au mabegi yako waone Nguo mpya au Mafuta au uwe na mizigo mingi ndio utajua.

Hivyo hivyo na Polisi, hapo Sijui ya Hospitali na kwingine.

MUHTASARI

Ni siku 500 zimepita tangu Rais John Magufuli aingie madarakani na kuteua timu ya watendaji wakuu katika sekta mbalimbali. Kipindi hiki kinatosha kuwapa wananchi mwenendo wa vitendo vya serikali na kuona jinsi ambavyo aina ya uongozi huu unavyoyagusa maisha yaoya kila siku

Muhtasari huu umebeba maoni ya wananchi juu ya masuala ya kisiasa. Kwa mtazamo wao, ni tatizo gani kuu linaloikabili nchi kwa sasa? Je, tatizo hilo limebadilika ukilinganisha na miaka iliyopita? Je, wananchi wanauonaje utendaji wa viongozi wao, akiwemo Rais? Na je, kuna mabadiliko yoyote katika kukubalika kwa vyama mbalimbali vya siasa katika kipindi cha miaka michache iliyopita?

Takwimu hizi zilikusanywa kati ya tarehe 31 Machi na tarehe 17 Aprili mwaka 2017.

Matokeo muhimu ni:

• Wananchi wametaja umasikini/hali ngumu ya kiuchumi kama tatizo kuu linaloikabili Tanzania kwa sasa.
• Idadi ya wananchi wanaotaja upungufu wa chakula kama tatizo kubwa imeongezeka.
• Idadi ya wananchi wanaotaja rushwa kuwa tatizo kubwa imepungua.
View attachment 524332

• Tofauti na miaka iliyopita, ni wananchi wachache wanaokubali utendaji wa viongozi waliowachagua mwaka 2017.

View attachment 524333

• Asilimia 71 wanaukubali utendaji wa Rais Magufuli.

View attachment 524338
View attachment 524343

• Asilimia 84 ya wananchi wanasema huenda watapiga kura kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020.

View attachment 524342

• Asilimia 63 wapo karibu zaidi na CCM kuliko vyama vingine.

View attachment 524344

• Idadi ya wananchi wanaofungamana na Chadema imeshuka tangu mwaka 2013.

View attachment 524345

Fuatilia mubashara > LIVE - Yanayojiri Makumbusho ya Taifa: Utafiti wa Twaweza kuhusu Vipaumbele, Utendaji na Siasa nchini
 
Back
Top Bottom