Utafiti wa Kilmo upate msukumo mpya katika awamu ya Rais Magufulu

Kwamhuzi

JF-Expert Member
Nov 15, 2014
1,762
401
Kilimo na sekta muhimu sana kwa watanzania walio wengi.Hususan asilimia sabini ya Watanzania wanategemea kilimo kama ajira yao.Hii ina maana kwamba ukiendeleza kilimo umeendelza asilimia sabini ya Watanzania.Kwa ujumla awamu zote zilizopita hazikutilia mkazo kilimo.ingawa kulikuwa na mikati mingi zikiwamo sera ambazo zilikuwa na nia ya kuwapa wakulima matumaini lakini sio hasa kuendeleza kilimo.Matokea yake ni kushuka kwa tija katika kilimo na hatimaye kuchangia asilimia tatu tu katika pato la taifa na kuongezeka kwa umaskini wa kaya.

Tangu Mhe.Rais aingie madarakani hatujasikia matamshi mazito yanaashiria kwamba ana mkakati madhubuti wa kuendeleza kilimo hasa utafiti wa kilimo.Ikumbukwe kwamba bila kuwa na tekinolojia nzuri,haiwezekani kuwa na tija kwenye kilimo.Kwa ujumla utafiti wa kilimo katika awamu zote zilizopita,isipokuwa awamu ya Mwl.Nyerere haukupata msukumo uliotarajiwa ili ku-support kilimo chetu.Funding iliendelea kupungua mwaka hadi mwaka kiasi cha kushangaza na mpaka kufikia leo hii ni kama serikali imejitoa kwenye utafiti kabisa,kitu ambacho ni national suicide.Ni ajabu kwamba trend hii iliendana na kuongezeka kwa ufisadi na wizi wa fedha za uma,kwa hiyo naamini kuna uhusiano.Katika hali ya kushangaza serikali iliendelea kusisitiza kwamba watafiti watafute fedha za utafiti kutoka kwa wafadhili,bila kujali usalama wa taifa.Naomba ikumbukwe kwamba utafiti ni eneo ambalo ni strategic kwa hiyo hatuwezi kuwaachia wafadhili.Sio vibaya wakituchangia,lakini lazima wafiti in our priorities.Ilivyo sasa ni kwamba sisi tuna-fit in their priorities,hii haikubaliki for purposes of national security.

Nimalizie kwa kusema kwamba pamoja na umuhimu wa kilimo na hasa kitengo cha kilimo,sijamsikia Mhe.Rais akitoa tamko lolote la jinsi ya kuendesha utafiti wetu katika utawala wake.Nadhani ni wakati muafaka sasa wa yeye kufanya hivyo.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Ndugu umezungumza kitu cha maana kabisa ambacho kinaweza kumfanya Magufuli akumbukwe na watanzania zaidi ya nusu katika utawala wake. Lakini kwa bahati mbaya watu wametega masikio nani anafukuzwa leo ama kutumbuliwa jipu. Matokeo yake huko vijijini kuliko na watanzania wengi watu wanaishi kwenye umaskini wa kutupwa. Huko ukienda mkulima hata uwezo wa kuweka tractor lilim heka 2 hamudu, achia mbali kuotesha mbegu duni. Ukweli ulio dhahiri iwapo Magufuli hatachukua hatua za msingi kwenye kilimo ataishia kuijenga Dar ili apate sifa toka vyombo vya habari, na baadhi ya miji inayoongozwa na wapinzani kama kete ya kuwapora wapinzani maeneo hayo ili yarudi ccm.
 
Back
Top Bottom