GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
- Wale watu wote wanaozaliwa kati ya saa 11 alfajiri hadi saa 2 asubuhi huwa ni wenye akili, wachapakazi wazuri na watu wanaojiamini na wanaofanikiwa kimaisha upesi sana.
- Wale watu wote wanaozaliwa kati ya saa 3 asubuhi hadi saa 7 mchana huwa ni watendaji wazuri sana ila wakali (wasiopenda mzaha mzaha) na kwamba hata watu wengi wenye uwezo wa kuwa viongozi huzaliwa mida hii.
- Wale watu wote waliozaliwa kati ya saa 8 mchana hadi saa 12 jioni huwa ni wavivu, omba omba sana na wadekaji wazuri na wanapenda kubebwa bebwa maishani.
- Wale watu wote waliozaliwa kati ya saa 1 jioni hadi saa 4 usiku huwa ni watu wakarimu sana, siyo wachoyo, wastaarabu na wanapenda mno kujichanganya na watu.
- Wale watu wote waliozaliwa kati ya saa 5 usiku hadi saa 10 alfajiri huwa ni wacha Mungu sana na msiojua wachungaji au makasisi au masheikh asilimia kubwa wengi wao huzaliwa mida hii na ni watu ambao wana nguvu mno ya kimungu ambapo hata wakisema wakuombee bado dua au ibada zao mwenyezi Mungu huzisikia sana.