Utabiri kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014

Utabiri kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa 2014

Chama cha mapinduzi tulisha kizoea kuwa 99% ya wanachama ni wachawi na wanajimu!! Ila saa ya shetani kutawala tanzania imefikia tamati!!
 
bora uchaguzi wa monita wa darasa kuliko huu unaozungumzia. tz imeonekana kama sudani kusini taifa jipya
 
Yani humu watu wa Lumumba wanajitekenya na kucheka wenyewe,Hahahahhh!!!
 
Mpaka muda huu Mwanza vituo vya kupigia kura havijulikani,wanasema vitatangazwa baadaye,
 
Kwani hilo nalo la kulitabiria? Nasikia JK ameshatupa jalalani mapendekezo mengi ya Bunge
Kwa taarifa yako wewe kada wa chama cha magamba, kama JK ataamua kuyatupa mapenekezo yote manane ya PAC, tafsiri yake ni kuwa atakuwa pia ameamua kuitosa 'indirect' jalalani CCM yake, na kuamua kukizika rasmi chama chake cha magamba, kwa kuwa kwa kuipinga ripoti ya PAC ambayo ni ripoti ya wabunge, ambao ni wawakilishi wa wananchi wote wa nchi hii.

Kwa maana hiyo kuikataa ripoti ya PAC, ambayo imetokana na ripoti za CAG na PCCB, ambapo vyombo hivyo vipo kwa mujibu wa Katiba ya nchi hii.

JK kukataa mapendekezo hayo ya Bunge, ambacho ndiyo chombo pekee cha wawakilishi wa nchi hii,tafsiri yake ni JK kuwafanya watanzania wote kuwa hawana maana na wapuuzi kabisa!
 
Mkuu Brightman,

Nafikiri hoja yako ina mashiko ingawa humu jamvini wengi wetu tunatanguiza hisia za uchama zaidi kuliko ukweli uliopo. Tunasahau kuwa hata tuweke hisia mbele kiasi gani ukweli utabaki daima

labda ambacho hukufanya ni kueleza vipi umefikia kiwango hicho cha ushindi pamoja na na kufafanua ni sababu zipi ambzo zingepelekea kuwepo kwa hali ambayo itakipelekea CCM kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mbao kwa mtazamo wangu kama matokeo yatakuwa kama alivyo ni ishara tosha kuwa mwaka 2015 wapinzani watapigwa mchana kweupe.

Uchaguzi huu ni muhimu zaidi kwa kuwa unajenga msingi wa uongozi wa ndani ya chama na ngazi ya serikali na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kuweka mikakati ya kuwezesha chama kupata ushindi, hivyo chama ambacho kitapata nafasi katik ngazi hii ambayo ndiyo iliyo karibu zaidi na wananchi, kina nfasi kubwa ya kuibuka na ushindi.

jambo moja nimebaini, taarifa ya idadi ya watu walijiandikisha kupiga kura za uchaguzi wa serikali za mita katika mkoa wa dar es salaam pekee, zinaonyesha kuwa ni asilimia 42 pekee ya wapiga kura ndio waliojiandikisha! kuna baadhi ya watu humu ndani hawakujiandikisha wakidai uchaguzi huu sio wa muhimu, wako busy N.K

jambo lenyewe ni hili, watanzania wanodai kuunga mkono vyama vya upinzani hufanya hivyo kwa mneo ya vijiweni na au kwenye mtandao lakini HAWAJITOI katika shughuli mbalimbali za vyama wanavyodai kuviunga mkono. Inawezekna unafahamu mifano mingi lakini kuna hili suala la waliojitokeza kuomba nafasi za uongozi kupitia Ukawa,nimebaini "wengi" hawana mvuto kwa wapiga kura kwa kuwa wale ambao wangetarajiwa kugombea wamebaki nyuma wakisubiri watu wengine walete mabadiliko yanayotarajiwa.

Inawezekana wagombea hao "wakashinda", lakini hii inaweza kusababishwa na "li-upepo" kuwa wananchi wanataka mabadiliko ya viongozi kutoka vyama vingine lakini sio mvuto kwa wapiga kura. Hata mapigamzi yanayodaiwa kuwa sababu ya wagombea wa Ukawa kuzuiwa yanayotoana na sababu iele ile ya wengi kuunga mkono vyama vya upinzani kwa maneno na sio vitendo!

Jambo moja na dhahiri viongozi wabovu huingia madarakani kutokana na wewe au mimi kushindwa kujitokeza kupiga kura au kupigiwa kura.
 
Kama mtaleta wapiga kura kutoka nje ya na mabox ya kura nakubaliana na wewe 100% lakini kama mtabanwa msiingize wapiga kura feki na hayo masanduku utabiri wako utakuwa wa viroba. Kwa hali ilivyo ccm mnahali mbaya sana. Mimi Jirani yangu ni ccm alinifata usiku akanipa ka escrow nikaona aibu nikakanywa sasa atajua pesa za escrow ni za umma au ni za magamba.
 
Kwa hali ilivyo mpaka sasa natabiri CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa 80%, ikifuatiwa na CHADEMA 12% na vyama vingine vitagawana 8%. Amini usiamini huu ndo utabiri halisi utakaotimia kuanzia tarehe 14,Desemba 2014. Mnaopinga tusubiri siku ifike!

ushind wa mapingamizi???????????
 
Kwa hali ilivyo mpaka sasa natabiri CCM itashinda kwa kishindo Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa 80%, ikifuatiwa na CHADEMA 12% na vyama vingine vitagawana 8%. Amini usiamini huu ndo utabiri halisi utakaotimia kuanzia tarehe 14,Desemba 2014. Mnaopinga tusubiri siku ifike!

Acha ujinga nina
Wasiwasi na elim yako pia uwezo wa kufikiri ni hafifu sana
 
Uchaguzi wa kidemokrasia Tz utafanyika mara tu yaliyo tokea Kenya yakifanyika ndipo tutakapo elewana kwamba wagombea na wapiga kura wote ni watanzania la sivyo nikama mambo yanayofanyika Zanzibar.
 
Hata ccm ikishinda kwa 100% haiwasaidii kwani imekuwa wazi kwamba sahivi mmebaki maadui hata vibibi vinawaadhibu na sehemu yoyote mtakapopita kwa hila mtegemee protests kutoka kwa wananchi throughout 5years non-stop
 
Bado unamhitaji hekima ya mungu uweze kutabiri kabla hujatabiriwa""""ccm chaliiiiiiii"""" na utabari wako feki:msela::msela:
 
Bado unamhitaji hekima ya mungu uweze kutabiri kabla hujatabiriwa""""ccm chaliiiiiiii"""" na utabari wako feki:msela::msela:

Subiri wewe mbona una haraka? Matokeo bado yanaendelea kutolewa!
 
Back
Top Bottom