Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 5,738
- 15,209
Amani iwe nanyi.
Ikiwa leo tarehe 16/7/2020 Waziri wa zamani wa mambo ya nje Mh Bernard Membe anatangazwa rasmi kujiunga na chama cha ACT Wazalendo ambapo bila shaka atapewa ridhaa ya kuwania urais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo mwezi October mwaka huu hivyo kuwa mshindani wa Rais Magufuli.
Kwa kumwangalia akiwa anaongea Bernard Membe inaonyesha ana uchungu sana na anataka kubadilisha kitu kwenye nchi hii, pia inaonyesha ndani ya moyo wake ameapa iwe mvua au jua lazima awe rais wa Tanzania!
Si jambo baya wala si uvunjifu wa katiba kuota kuwa rais wa Tanzania kama anavyofanya Membe lakini unatakiwa ujitafakari ni wakati gani hiyo ndoto unatakiwa uiote.
Kama mwaka 2015 Membe aliweza kupenya tano bora na Magufuli na akashindwa mbele ya kaka yake Jakaya Kikwete basi kwenye uchaguzi wa mwaka huu 2020 hataweza kumtikisa Magufuli hata kipande cha unywele wake. Inawezekana kweli wapo vigogo wanaomshawishi na kumhakikishia Membe kuwa atashinda urais hapo October na kutawazwa kuwa rais wa Tanzania lakini naomba nimwambie ukweli hao vigogo wamelenga kumlia hela zake tu.
Membe kaa utulie ulee wajukuu ,habari za kuwa rais wa Tanzania zimeshapita na hazitakurudia tena.