Utabiri - Barcelona haitatwaa ubingwa wowote msimu huu

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
125,780
239,458
Baada ya kutamba kwa kipindi kirefu kwenye soka la vilabu duniani hatimaye barcelona imeishiwa pumzi .

dalili za pumzi kukata zilianza kujionyesha pale walipohenyeshwa na timu mbovu na isiyo na mkakati wowote ya Arsenal kwenye ligi ya mabingwa ( hata kama walishinda ).

ukweli ulijidhihirisha katika ELCLASSICO walipopigwa nyumbani na wachezaji kumi tu wa Real Madrid na jana wameangukia tena pua kwa kibonde Real Sociedad na hivyo kuongoza ligi kwa tofauti ya point 3 tu !

Kuporomoka huku ni dalili ya kuanza safari mpya ya kuwa Timu Mdebwedo.

Kwaheri Barca , maisha ndio yalivyo .
 
sasa kama unapigwa na Real sociedad utamfunga nani tena ?
hawatachukua kombe lolote?
hii post yako imekaa kihisia zaidi kuliko kiuchambuzi, labda ungesema "inaweza isichukue kombe lolote " ingeonekana smart kidogo
Barcelona wanaongoza ligi ambayo inakaribia kuisha kwa point 3, copa del rey wapo hatua za mwishoni na Uefa wapo robo fainali, na tayari wameshashinda nyumbani
sasa ni mtu gani atasema haitachukua lolote?
hilo la kufungwa na real sociedad linatokea, ile ni ligi na kuchukua ligi haimaanishi ufunge kila timu kibonde,
 
Ubingwa wa League sasa ni open. Vipigo viwili mfululizo sasa vimewarudisha Real Madrid kwenye game. Ila Barcelona wataambulia angalau kombe moja (Copa de rey..)
 
Inaelekea wewew sio mfuatiliaji wa soka barc kupoteza mechi mbili za ligi sio kwamba kaishia pumzi Iko hivi
Barcelona vs real Madrid
Hapa Barcelona waliingia uwanjani ila akili zao zilikuwa katika game ya atletical ambayo ukifungwa umefungwa(kumbuka ligi walikuwa mbele kwa point 7 dhidi ya atletical na kumi dhidi ya real)

Real socciedad vs Barcelona
Hapa hakuna ubishi tangu mwaka 2007(kama sikosei) Barcelona hakuwah kumfunga huyu jamaa ugenini


Nilipoona hii thread nikajua utakuwa umechambua vizur ila upo kiushambiki zaidi
sasa kama unapigwa na Real sociedad utamfunga nani tena ?
 
Mimi si mshabiki wa Barca ila barca hafanyi vizur pindi anapocheza na reak sociedad yaan huwa inamsumbua saana kwa hyo hicho sio kipimo cha kuipima barca na makombe
 
Mimi si mshabiki wa Barca ila barca hafanyi vizur pindi anapocheza na reak sociedad yaan huwa inamsumbua saana kwa hyo hicho sio kipimo cha kuipima barca na makombe
hapa nazungumzia mwenendo mzima wa barca mkuu , hali si shwari .
 
Hebu nenda kwanza ukatafute kwa mara ya mwisho Barca iliifunga Real Sociedad lini huko kwao?
Big up man.. Mleta mada anabonga tu.. Hata historia hajui. Hili ni tatizo la kujadili soka na watu walioanza kushabikia soka mwaka jana.
Barca ni dhaifu sana kwa hii timu ya Real Sociedad hasa wakiwa kwny uwanja wao. Hii si ticket ya kusema kwamba ubingwa bas. Mpira unadunda mwn
 
Inaelekea wewew sio mfuatiliaji wa soka barc kupoteza mechi mbili za ligi sio kwamba kaishia pumzi Iko hivi
Barcelona vs real Madrid
Hapa Barcelona waliingia uwanjani ila akili zao zilikuwa katika game ya atletical ambayo ukifungwa umefungwa(kumbuka ligi walikuwa mbele kwa point 7 dhidi ya atletical na kumi dhidi ya real)

Real socciedad vs Barcelona
Hapa hakuna ubishi tangu mwaka 2017(kama sikosei) Barcelona hakuwah kumfunga huyu jamaa ugenini


Nilipoona hii thread nikajua utakuwa umechambua vizur ila upo kiushambiki zaidi
Mkuu naona kama umepitiwa hapo kwenye 2017!!
 
Mtoa mada hizo ni hisia zako tena zimekaa kishabiki mtu anaongoza ligi unaanza utabiri huo utabiri au maombi yako ya usiku umeanza lini kua mtabiri wa Barca utabiri wako wenyewe hasi tu mbona wakiwa wanachapwa watu hatuoni utabiri wa Mema dhidi ya Barcelona Mwambie Wenger akomae na top 4 bana Barca huiwezi ndugu
 
viroba ni hatari kwa afya ya vijana hii ni pointless viva barcelona wazee wa trebo
 
-Barca yupo fainali dhidi ya Sevila mwezi ujao.

-Game ngumu ilibaki kwa Barca ilikuwa ni ya Jmos dhidi ya Sociedad sababu tangu 2007 Barca hajawahi beba ushindi uwanjani hapo. Hata akipoteza mchezo mwingine bado League ataongoza.

-Barca bado ana nafasi UEFA kusonga mbele, na endapo Real Madrid akitoka, kombe linarudi tena Barca.


-Arsenal mpaka sasa mnapigania kombe gani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom