Usumbufu wa daladala Eneo la Mwenge Mabucha

mnyakwetu

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
309
96
Kumekuwa na usumbufu mwingi kwa hizi daladala zinazopita barabara ya TRA kwenda Sinza,Shekhilango,Mabibo hususani eneo la Mwenge Mabucha kona ya kuingia sokoni, wamefanya ndio Stand ya kupaki wakati stand yao kiko kule baada ya Taa za Mwenge kwenda Coca-cola.

Mwanzoni Trafic wa Mwenge walikuwa wanawatimua lakini kwa sasa wamewaacha kabisa waendelee kusababisha usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara hii, nimejaribu kuongea nao wanasema Trafic hawawezi kuwatoa kwa sababu Trafic wana share zao hapo.

Ikiwa ni kweli jambo hili basi mkuu wa kituo cha Police Mwenge anapaswa kuwajibika katika hili. Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom