Usomi dhidi ya Elimu = Ujinga wetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usomi dhidi ya Elimu = Ujinga wetu

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kigarama, Jun 28, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tangu tuingie kwenye utandawazi na siasa za vyama vingi hapa Tanzania kila mtu anataka kuonekana msomi. Siku hizi kuna vyuo vikuu vingi sana hapa nyumbani (vingine uchwara) ambavyo watanzania wengi wanasoma huko. Lakini jambo pekee linalojitokeza kwenye jamii yetu tuko makini sana kuwa wasomi bila ya kujali kama tunaelimika.

  Tunao wasomi wengi wa nyanja mbalimbali lakini mpaka sasa wengi wao wameshindwa kututhibitishia kama usomi wao unaendena na elimu iliyokusudiwa. Kila mtu anataka kuwa msomi, lakini ni wangapi wetu leo hii tunataka kuelimika? Hapo ndipo tulipokwama.Mtu ana shahada ya Uzamivu (PHD) anawezaje kusaini mkataba feki? Siasa zetu na uchumi wetu hauwezi kubadilika bila ya kuwa na wasomi wenye elimu ya kutosha.

  Samahani kwa kutumia lugha ya KIswahili ambayo si ya kisomi.
   
 2. Averos

  Averos JF-Expert Member

  #2
  Jun 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 648
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Kumbe kusoma na kuelimika ni vitu 2 tofauti!
   
Loading...