SoC02 Usiyoyajua: Mazingira saba (7) hatarishi kwa mwanachuo

Stories of Change - 2022 Competition

Elisha Jilala

New Member
Jul 26, 2022
2
4
Utangulizi

Ni ukweli kwamba wanafunzi wengi wanaomaliza kidato cha sita na wale wanaosomea fani vyuo vya kati na vyuo vya ufundi wamekuwa na ndoto kubwa za kufika elimu ya juu yaani chuo kikuu. Ndoto zao hukubwa na misukosuko huku wengine wakikatiza masomo yao pale changamoto zinapozidi uwezo wao. Japo changamoto humuinua mtu na kumuimarisha, zipo pia changamoto ambazo hugeuka kuwa mwiba na adui wa maendeleo ya kitaaluma kwa mwanafunzi wa elimu ya juu. Makala hii inakuletea maadui saba wa mwanachuo, makala hii itamsaidia mwanafunzi, mzazi na mlezi kuyajua mazingira hatarishi kwa mwanachuo awapo chuoni.

Wanafunzi wa chuo ni kundi ambalo limekuwa likilengwa na vitendo vya wizi na utapeli. Inafaahika kuwa, wanafunzi wa chuo hupokea pesa ya kujikimu (boom) kila baada ya siku 60. Hali hii huwaweka hatarini dhidi ya mashambulizi ya wezi, matapeli na vibaka. Tafiti zinaonesha; wanafunzi wa chuo huibiwa pesa, simu, laptop na hata nguo huku wezi wakitoka mitaani na wengine hutoka ndani ya chuo (wanafunzi kuibiana wenyewe kwa wenyewe).

Wanafunzi huibiwa wawapo maeneo ya chuo na hata nje ya maeneo ya chuo. Wawapo maeneo ya chuo huibiana wao kwa wao huku vitendo hivyo vikifanyika usiku. Pia vifo vingi vinavyoripotiwa vyuoni vimelezwa vyanzo vyake ni pamoja na ajali za barabarani, wivu wa kimapenzi, magonjwa, ugomvi na sababu nyinginezo. Makala hii imesheheni mambo mengi mazuri ambayo yatamjuza na kumfahamisha mwanafunzi juu ya mazingira hatarishi awapo chuoni

1. Bwenini (Hosteli)
Mwanafunzi afikapo chuoni hukabidhiwa chumba cha kulala, kwenye hostel za chuo zilizozungukwa ukuta na ulinzi mkali kutoka katika kampuni mbali mbali za ulinzi kama vile SUMA JKT, ULINZI JKT nk, mara nyingi vyumba hivyo huwa na vitanda na makaabati ya kuhifadhia vifaa vya wanafunzi. Chumba hizo huweza kuwa na idadi ya wanafunzi wawili na zaidi. Katika hali isiyo ya kawaida, wanafunzi humuibiana wao kwa wao vitu kama simu, laptop, nguo na pesa.

Pia, mwanafunzi kutoka chumba huondoka chumbani kwake na kuingia chumba jirani huku akitekeleza adhima yake chafu ya wizi.

Mbinu nyingine ambayo hutumiwa ni kupitia funguo za mlango husika. Vyuo vingi baada ya mhula wa mwisho wa masomo kumalizika wanafunzi hurudisha funguo kwa watunza bweni (wadens) wanafunzi wasio waaminifu huchonga funguo zingine na kubaki nazo. Chuo kinapofungulia chumba hicho hukabidhiwa kwa mwanafunzi mwingine. Mwanafunzi huyo asiye na nidhamu huenda chumba husika either mchana au usiku na kufungua kisha kuiba mali za wanafunzi wenzake ikiwemo simu, komputer na pesa.

Kati ya tukio lililogonga vichwa vya habari kwa chuo Kikuu cha Dar es Salaam ni tukio la mwanafunzi kufariki baada ya kujaribu kuiba laptop katika chumba cha wanafunzi wenziye. Baada ya kuingia ndani wenye chumba hicho walishituka hali iliyomfanya mwanafunzi huyo kuruka kutoka ghorofa ya pili mpaka chini hali iliyomsababishia majeraha makubwa mpaka u mauti.

2. Sehemu za usafiri wa umma
Hizi ni sehemu zinazohusisha vyombo vya usafiri wa umma ikiwemo daladala, mwendokasi, train nk. Sehemu za usfairi huwa kuna msongamano na mbanano mkubwa wa watu, wezi hutumia nafasi hiyo kuchomoa na kufungua mabegi ya abiria wenzao na kuiba simu, waleti, nk. Mwanafunzi wa chuo kikuu anapowasili chuoni... mambo mengi huwa ni mageni kwake hivyo kushindwa kuwa na tahadhari hasa anapopanda vyombo vya usafiri.. hali hii humuweka katika mazingira hatarishi ya kuibiwa.

3. Sehemu za starehe
Sehemu za starehe kama vile baa, nisemehe zilizoripotiwa kama sehemu hatarishi kwa wanafunzi wa vyuo. Matukio ya wanafunzi kuwekewa vilevi vikali na kuibiwa ni matukio ya kawaida kwa maeneo yanayozunguka vyuo vikuu.

4. Maeneo za makazi yao
Wanafunzi wengi hupanga vyumba mtaani hii ni kwasababu ya uwezo mdogo wa chuo kutoa huduma za hostel kwa wanafunzi na pengine ni vipaumbele na mitindo ya maisha wa wanafunzi. Tafiti zangu zinaonesha wanafunzi wa vyuo vikuu wamekuwa wakiimbiwa sehemu za makazi yao either kwa kuvamiwa, kuchanwa madilisha yao na kuibiwa huku wengine wakianuriwa nguo zao walizokuwa wamefua.

5. Chuma ulete
Japo wengi hawaamini katika ushirikina na uchawi, tafiti zangu zimeonesha wazi kuwa, wanachuo wengi wametapeliwa na kuibiwa katika hali isiyo ya kawaida. Mwanafunzi mmoja alieleza kwa masikitiko kuwa, aliombwa chenji na mtu asiyemjua, kwenye waleti yake alikuwa na shilingi elf 56 baada ya kumpatia chenji yule mtu alitembea hatua chache tu, alitoa waleti yake ili anunue maji kwaajili kutibu kiu iliyokuwa ikimsumbua. Baada kuangalia kwenye waleti yake hakukuwa na pesa ya aina yoyote. Pia matukio kadhaa yamelipotiwa ya wanafunzi kushikana mikono ama kuguswa na watu wasiowajua hali iliyowafanya kupoteza kumbukumbu na kukabidhi kila kitu kwa watu hao.

6. Sehemu za mabenki na ATM
Ni ukweli usiopingika kuwa kwenye mabenki na ATM nyingi pamejaa ulinzi mkali wa askari na CCTV camera, lakini mbinu zinazotumiwa na wezi zinaacha watu midomo wazi. Mwanafunzi mmoja wa chuo kimoja kilichopo jiji Dar Es Salaam alisimulia kisa chake cha kuibiwa ATM katika hali isiyo ya kawaida.
Akiwa mwaka wa kwanza, ujumbe wa maandishi uliingia kwenye simu yake huku ukimfahamisha “kiasi cha shillingi laki saba za kitanzania ziliingizwa kwenye akaunt yake” hii ni baada ya kusaini pesa zake za kujikimu. Kwa sababu ya shauku na ugumu wa maisha alioupitia alienda haraka ATM za chuo ili kuweza kutoa fedha kiasi kwaajili ya matumizi yake binafsi. Kwa bahati mbaya ATM iliyokuwa karibu na maeneo ya chuo ilikuwa haifanyi kazi, aliamua kwenda mtaani ili akatoe pesa. Wakati anaingia ATM mtu mwingine aliingia kwani kulikuwa na ATM machine mbili kwenye chumba hicho. Hakuwa na wasi wasi kwani kwa nje kulikuwa na mlinzi. Yule mtu alimsemesha na kumtaka amsaidie kama anapitia changamoto. Alimkabidhi kadi ya benki na kumtajia namba ya siri. Alichomeka ile kadi na kuandika namba ya siri. ATM machine iligoma na kutoa ujumbe kuwa namba ya siri ni batiri. Yule mtu aliondoka na kumuacha yule mwanafunzi akihangakika. Hakupata msaada na hivyoa aliamua kuondoka na kwenda kufatilia ili kubaini chanzo cha tatizo, katika hali ya kustaabisha aliambiwa pesa zote zimetolewa.

Mbinu iliyotumika; yule mtu alichukua kadi ya mwanafunzi huyo huku akiwa na kadi inayofanana na yake, baada ya kufahamu namba ya siri basi akachomeka kadi ambayo siyo ya yule mwanafunzi, ujumbe wa kuweka namba ya siri batili ndiyo ilikuwa ricket yake ya kuondoka na kumuacha mwanafunzi huyo akihangaika huku akiondoka na kadi ya benk ya mwqnafunzi huyo na kwenda kutoa pesa hizo sehemu nyingine

7. Biashara mtandao (GLOBAL ALLIANCE, Q NET nk)
Mbinu zingine zinazotumika kuwalaghai wanafunzi wanaojiunga na elimu ya juu ni utapeli, ambapo mwanafunzi hushawishiwa kuingia kwenye vikundi na biashara mtandao zinazohitaji kuchangia kiasi cha pesa huku akitarajia matunda makubwa. Baada ya kuchangia watu hao hupotea na kutokuonekana kusikojulikana.

Nini kifanyike kukwepa au kuepuka hali hii?
Usimwamini kila mtu unayekutana naye, pengine unaweza ukawa na moyo mzuri wa kumsaidia mtu; kumwelekeza mahali. Kupitia huo wema wako mtu mwingine anaweza tumia hiyo nafasi kukuibia au kukudhuru.

Usikubali ofa ya kinywaji wala lift ya gari kwa mtu usiye mjua. Pia usipokee hata mkono wa salam kwa mtu usiye mfahamu. Ni kheri kukaa kimya kuliko kuonekana unajua kuongea na mtu usiyemjua.

Ununuapo vitu, hakikisha una nunua dukani. Au kwa mtu ambaye ana vielelezo kuwa ile mali ni yake. Kesi nyingi zimewakuta wanafunzi kwa kununua simu za wizi zilizotumika katika uhalifu kama vile ugaidi, mauaji na biashara haramu.

Hifadhi vitu vyako sehemu nzuri na yenye usalama wa kuaminika, kama una kabati ndani ama hata begi la kufunga, basi weka vitu vyako na fungia ndani. Hii itakusaidia hata kama mtu ataingia chumbani kwako kwa funguo bandia, vitu vyako vitakuwa salama vikiwa vimefungiwa kwenye kabati au begi.

Funga mapazia na madirisha kisha zima taa kabla ya kulala, kwani ukilala taa zinawaka inakuwa ni rahisi kwa mtu kuona vitu vilivyomo ndani na kukuibia kiurahisi. Kama utaacha dirisha wazi hasa kwa madirisha ya vioo, weka kitanda chako mbali na dirisha au hifadhi vitu vyako kama vile simu, laptop na waleti mbali na dirisha, hii itakuepusha kuibiwa kwa urahisi.

Vaa nguo ya kubana kidogo kama vile jinzi pale unapopanda magari ya umma kama ile daladala na mwendo kasi hii itakusaidia kuvihisi (sense) vitu ulivyovibeba na kutambua kiurahisi pale mtu yoyote atakapojaribu kukuchomolea. Kama utavaa nguo za kupwaya basi vitu kama waleti na simu shikilia mkononi. Na kama utabeba begi, shika mkononi au livae mbele ya kifua chako. Matukio mengi yameripotiwa; mabegi kufunguliwa na kuibiwa vitu vya thamani.

Kama utaends kutoa pesa kwenye ATM yoyote na ukapata changamoto, muulize askari aliyevalia sare karibu na eneo hilo. Usiulize mtu usiye mjua

NI MATUMAINI YANGU KUWA MAKALA HII ITAKUWA MASAADA KWA WANAFUNZI NA WAZAZI WENYE WATOTO WAO WANAOTARAJIA KUJIUNGA NA MASOMO YA CHUO KIKUU NA HATA WALE WANAOENDELEA NA MASOMA
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom